Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Makao Makuu tarehe 12/2/2016 imewafikisha washtakiwa
wafuatao mahakamani, ambao pia ni maafisa waandamizi wa Shirika la Reli Tanzania
(TRL):
1. Kipalo Amani Kisamfu,
Mkurugenzi Mkuu wa TRL
2. Jaspar hurbert Kisiraga,
Mhasibu Mkuu wa TRL
3. Mathias Andrew
Massae
4. Muungano Gabriel
Kaupunda
5. Ngoso Joseph
Mwakilembe Ngosomwiles
6. Pascal John Mafikiri
7. Kedmon Peter Mapunda
8. Felix Rwezaula
Kashaigili
9. Lowland Watson
Simtengu
10. Josepth Mlinda
Syaizyagi
11. Charles Florence
Ndenge
Washitakiwa hawa wakiwa
Maafisa Watendaji Wakuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) wanadaiwa kutumia
madaraka yao vibaya na kutumia nyaraka kumdanganya Mwajiri kinyume na kifungu
cha 22 na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka
2007.
Kwa nyakati tofauti
washitakiwa wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya na nyaraka kwa kuipatia
zabuni Kampuni ya HINDUSTHAN ENGINEERING
AND INDUSTRIES ambayo haikukidhi vigezo, kuleta mabehewa ya kokoto nchini.
Fedha ambazo
zimeshalipwa kwa Kampuni ya HINDUSTHAN ni dola za kimarekani 1,280,593.75 kati
ya dola 2,561,187.50
Washtakiwa wamefikishwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kufunguliwa kesi namba 49/2016 inayosimamiwa
na Mhe. Hakimu Mchaura. Kesi imepangwa kusikilizwa tarehe 25/2/2016.
IMETOLEWA
NA OFISI YA AFISA UHUSIANO
TAKUKURU,
MAKAO MAKUU
12February 2016
Viongozi wa wa Kampuni ya Reli nchini Tanzania (TRL), wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam kusomewa mashitaka 9 yanayowakabili likiwemo la tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, wa pili kulia ni aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika hilo, Mhandisi Kapallo Kisamfu.
PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA
PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA
No comments:
Post a Comment