Ray C amekanusha tetesi zilizoanza kuenea kuwa amerejea tena
kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.
Hivi karibuni magazeti ya udaku yamekuwa yakiripoti kuwa
muimbaji huyo amekuwa akionekana kwenye machimbo ya uuzaji wa dawa hizo jijini
Dar es Salaam.
Kupitia Instagram, Ray C ameandika maneno haya kukanusha
habari za uongo:
Seriously kwa kweli huwa naumia sana sana kuona binadam
mwezangu anadiriki kuniharibia jina langu ilj yeye apate kula!hamjui mnaniathiri
kiasi gani na hizi habari zenu?Hivi unadirikije kuandika usengwile kama huu
bila hata aibu wala picha ya kuisapoti hiyo habari yani ni ujinga ujinga tu
umeunganishwa na picha yangu bila hata uoga mmeichukua kutoka kwwnye page yangu
ya insta bassss tayari mmeshapata story ili mradi tu mniharibie maisha yangu
ili nyie mpate pesa mi nife maskini!!!kama kweli mnauhakika na mlichoandika
kwanini hamkuweka picha yangu nikivuta hayp maunga badala yake mnaweka picha ya
kituo cha mkunguni ambapo madaladala husimamisha kituoni hapo.
Mmepiga picha ya kituo cha mkunguni mkaona haitoshi mkaingia
kwwnyw page yangu ya insta na kuchukua picha yangu niliojipiga mwenyewe ndio
mnazitumia kunichafulia jina langu tena wakati ndio kwanza nahangaika kurudi
tena kwenye kazi yangu. Haki amungu sijawahi kuskia hata siku moja nyie global
mmeandika kuhuau foundation yangu na mambo mazuri iliofanya,jw mnajua kama
mpaka sasa nimeshatoa vijana zaid ya sabini kwenye madawa na wako fit wanatumia
methadone je mnajua hilo?
Hata siju moja sikawahi pata msaada wowote kutoka kwenu japo
kunichangia nauli tu ya kuja kwenye dawa kila siku hakuna hata anaenisaidia huu
mwaka wa tatu bado naendelea kunywa dawa na ni kila siku ya mungu siku saba kwa
wiki hakuna sikukuu wala msiba na ukikosa mwili unauma vibaya sana yani its not
easy but am a fucking hard working woman na ni mwanamke jasiri napambana na
siogopi kujaribu,naparangana na haya madawa na nayapinga na kamwe sintorudi
nyuma na hizi nuksi mzipeleke kwenye familia zenu.
Wewe shigongo unamkosea sana mungu!unajifanya mlokolw lakini
kazi yako ni kuharibia maisha ya wenzio unasahau kuwa malipl ni hapahapa
duniani!Mimi ni kapuku tu sina mbwlw wala nyuma mbele yako lakini bado
unanichimbia kaburi angali mi mzima.Na wewe Mayasa Marwata ni mpuuzi usie jua
kazi yako!nimeisoma stori yako nimegundua ni mvivu Wa kufatilia habari!eti
Chimbo LA unga langu lajulikana sasa kama ushalijua mbona haukunipiga nikivuta
huo unga unaenda kupiga pixha kituo cha daladala bwege we! Ntapambana na nyie
MAHAKAMANI.
No comments:
Post a Comment