Pages

Sunday, February 14, 2016

SACIDS na OHCEA zawakutanisha wataalamu wa Afya kujadili mpango kazi wa pamoja‏

Dk. Deo Mtasiwa Naibu Katibu Mkuu wa Afya TAMISEMI akizungumza katika mkutano wa Afya Moja ulioshirikisha wadau mbalimbali wa Afya ya Mifugo, Binadamu na Mimea kutoka katika vyuo mbalimbali hapa nchini.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog).
Mhadhiri na mtafiti mtoa huduma katika chuo kikuu cha Sokoine, Profesa Robson Mdogera akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kuhusu mafanikio pamoja na changamoto wanazozipata kwenye mango wa Afya Moja wanapotaka kufanya kazi kwa pamoja kati ya madaktari wa afya ya mifugo, binadamu pamoja na aafya ya Mazingira.
Dk. Kitua kutoka SACIDS akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Wataalamu wa Afya kutoka vyuo mbalimbali hapa nchi ili kujadili nikwa jinsi gani wanaweza kushirikiana katika kufanya kazi bila kuangalia kuegemea upande wowote wa Afya.

  DSC_0017 DSC_0008Profesa Mamuya kutoka MUHAS akiwasilisha mada kwenye mkutano uliowashirikisha wataalamu mbalimbali wa afya ya mifugo, binadamu pamoja na afya ya mazigira uliofanyika Bagamoyo.
DSC_0023Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine kitengo cha Tiba ya Afya ya Jamii Dk. Helena Ngowi akiwasilisha mada mbele wataalamu mbalimbali wa Afya kutoka kwenye vyoa vya hapa nchini waliokuwa wanajidilini kwa jinsi gani wanaweza kushirikiana katika kufanya kazi.
DSC_0038Profesa Rudovick Kazwala kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) akichangia mada kwenye mkutano wa wadau wa Afya moja uliowashirikisha wataalamu mbalimbali wa Afya kutoka vyuo mbalimbali vya Tanzania.
DSC_0044Mhadhiri na mtafiti mtoa huduma katika Chuo Kikuu cha Sokoine, Profesa Robson Mdogera akizungumza jambo walipokuwa wanajadili mpango kazi wa pamoja ili kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kufanya bila kubagua upande wowote.
DSC_0134Profesa Mark Rweyemamu akizungumza jambo wakati wa kuwasilisha mpango kazi wao ili kuweza kuutumia kwa pamoja na kuachana na mpango wa kila kundi.
Makundi ya wataalamu mbalimbali wa Afya Moja wakijadili pamoja na kubuni mpango utakaowasaidia wataalamu wa Afya ya Mifugo, Binadamu pamoja na Mazingira kufanya kazi kwa pamoja yaani Afya Moja.
DSC_0205Profesa Rudovick Kazwala akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasimi aliyefika kufunga mkutano huo.
DSC_0211Picha ya pamoja.


Taasisi za SACIDS na  OHCEA wameandaa mkutano uliowakutanisha wataalamu mbalimbali wenye ujuzi tofauti wa Afya hasa Afya ya Mifugo, Afya ya Binadamu pamoja na Afya ya Mazingira kutoka kwenye vyuo mbalimbali vya hapa Tanzania.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuweza kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kufanya kazi kwa pamoja bila kubagua upande wowote ili kutatua tatizo lililokuwepo kwa miaka mingi hapa nchini Tanzania hasa pale yanapotokea magonjwa yanayowapata mifugo pamoja na binadamu.
Mgeni rasmi aliyefika katika mkutano huo alikuwa Dk. Deo Mtasiwa ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Afya TAMISEMI ambaye alisema kuwa serikali iko pamoja na wataalamu wa Afya ya Mifugo, Afya ya Binadamu pamoja na Afya ya Mimea.
Pia amesema mpango ulioandaliwa na wataalamu hao wa afya wa kufanya kazi kwa pamoja utachukuliwa na serikali ili kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kuutumia ili ikitokea ugonjwa kwa mifugo kwenda kwa binadamu iwe ni rahisi kutatua tatizo hilo.
"Magonjwa ya kuambukia yanayotoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu yanaleta changamoto kubwa sana lakini kwa sababu umekuwepo mpango wa Afya mmoja basi utatusaidia na pia tutawatumia wataalamu bila kuangalia yuko kundi gani," alisema Naibu Katibu Mkuu
Pia alisistiza kuwa umoja wao ndio mafanikio yao kwani wasipoungana na kufanya kazi kwa pamoja itakuwa ni vigumu kufikia yale malengo waliyojiwekea. "Napenda kuona mnatoa elimu katika jamii kuhusu magonjwa ya kuambukizwa ambayo yanatoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu ili kuweza kunusuru maisha ya wananchi walio wengi.
Pia alisema serikali iko tayari kuwasaidia kwa pale watakapohitaji msaada wao kwa sababu afya ni kitu cha msingi kwa wanyama pamoja na binadamu na kuongeza atashirikiana bega kwa bega na wizara kama vile Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Wizara ya Kilimo na Ufugaji ili kuweza kufikisha kile walichomtuma kama mtendaji wa serikali.
Pia ameshukuru taasisi zilizofanikisha mkutano huo ambazo ni OHCEA na SACIDS zimetengeneza mipango mizuri kwa wataalamu wa afya na kuwaleta karibu kwa ajili ya kushirikiana.
Akizungumza Profesa Robson Mdogera ambaye ni mhadhiri na mtafiti mtoa huduma katika Chuo Kikuu cha Sokoine amesema mkutano huu umekuja wakati muhafaka kwani kumekuwepo tatizo kubwa la kutoshirikiana katika hali zote.
“Huu mpango waliokuja nao wa Afya moja unaweza kuleta mafanikio makubwa maana kuna viwatilifu vinavyowekwa kwenye mifugo au mazao ili kukinga magonjwa hivyo kunapelekea viwatilifu hivyo kuliwa na binadamu bila kujua na kupeleka adhari kubwa katika mwili wa binadamu. Hivyo kunahitaji kuwa na ushirikiano katika nyanja zote za afya ili kuweza kutatua tatizo pale tu linapotokea,” alisema Prof. Mdogera.

No comments:

Post a Comment