Njile Gonga (28)
Huyu ndiye Jangili anadaiwa kutungua helkopta katika pori la Akiba la Maswa
lililopo katika Wilaya ya Meatu Mkoani, ambapo katika tukio hilo rubani wa
helkopta hiyo Rodgers Gower (37) raia wa uingereza huku Mwenzake Nicholas Beste
(43) raia wa Afrika Kusini akinususrika kifo.
Iddy Mashaka (49) ambaye ndiye alikuwa Mkuu wa kitengo cha
Interejensia katika hifadhi ya taifa Ngorongoro, ambaye anadaiwa kuwa
kiunganishi Mkuu wa kutekeleza tukio la kutunguliwa kwa helkpta hiyo.
|
Hali ya ulinzi na usalama ilivyokuwa imehimarsihwa
mahakamani pamoja na kituo cha polisi Bariadi.
|
Watuhumiwa wakiwa ndani ya gari la polisi, baada ya
kufikishwa kituo cha polisi Bariadi wakitokea wilayani Meatu kwa ajili ya
kufikishwa mahakamani.
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Elaston Mbwilo akionyeshwa watuhumiwa
wa ujangili ambao walihusika kutungua Helkopta.
|
Iddy Mashaka (49) ambaye ndiye alikuwa Mkuu wa kitengo cha
Interejensia katika hifadhi ya taifa Ngorongoro, ambaye anadaiwa kuwa
kiunganishi Mkuu wa kutekeleza tukio la kutunguliwa kwa helkpta hiyo.
|
Watuhumiwa wakiwa Mahakamani.
|
Watuhumiwa wa tukio la kutungua ndege aina ya Helkopta na
kumuua rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza lilitokea mnamo tarehe
29/01/2016 katika pori la akiba Maswa wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, leo (jana)
wamefikishwa mahakani kusomewa mastaka yanayowakabili.
Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama ya Mkoa wa
Simiyu, chini ya ulinzi wa mkali wa askari polisi, huku umati mkubwa wa
wananchi wa mji wa bariadi waifurika kushuhudia watuhumiwa hao.
Akiwasomea mashtaka watuhumiwa hao Wakili mwandamizi wa
serikali Mkoa wa Simiyu Yamiko Mlekano alisema kuwa washitakiwa wote 9
wanakabiliwa na kesi tatu ambazo ni Uhujumu uchumi, mauaji pamoja na umiliki wa
siraha bila ya kibali cha serikali zenye mashtaka tofauti.
Katika kesi ya Uhujumu uchumi iliyosomwa chini ya Hakimu
mkazi mfawidhi mwandamizi wa mahakama hiyo John Nkwabi katika shtaka la kwanza
mtuhumiwa namba moja Iddy Mashaka (49) anatuhumiwa kujihusisha na kuratibu
tukio la uhujumu uchumi kinyume na kifungu 4(1)(d) sura (57) (1) na 60 (2) cha
makosa ya uhujumu uchumi sheria namba 200 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mlekano alisema kuwa katika kosa hilo mshitakiwa kati ya
tarehe 6 januari na 1/02/2016 katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu aliwashauri
Mshitakiwa namba mbili Shija Mjika (38) kuua wanayama wasiyoruhisiwa kama
tembo.
Katika shtaka la pili wakili huyo aliwataja watuhumiwa namba
mbili hadi tisa ambao ni Shija Mjika (38) Njile Gunga (28), Dotto Pangali (42)
Moses Mandagu (48) Dotto Huya (45), Mwigulu Kanga (40) Mapolu Njige (50) pamoja
na Mange Barumu (47), watuhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi.
Katika shtaka hilo wakili aliieleza mahakama kuwa kati ya
tarehe 21/01/2016 na 29/01/2016 katika wilaya ya Meatu, watuhumiwa hao
walipanga na kuratibu tukio la kuwinda wanyama aina ya tembo bila ya kibali cha
serikali.
|
Hata hivyo wakili huyo alieleza kuwa katika shtaka la tatu
watuhumiwa
namba mbili hadi tisa waliotajwa hapo mwanzo, watuhumiwa
kujihusisha na uwindaji wa wanyama wasiyoruhusiwa kinyume na kifungu 47(a)(aa)
cha sheria namba 5 ya mwaka 2009 sambamba na sura 14 (a) na kifungu 57 (1) cha
uhujumu uchumi sura 200 iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Alisema katika shataka hilo mnamo kati ya tarehe 26/01/2016
na 29/01/2016 katika hifadhi ya Mwiba katika kijiji cha Makao wilayani Meatu
watuhumiwa walimuua tembo mwenye dhamani ya shilingi Milion 32,891,100 bila ya
kibali cha serikali.
Katika shtaka la nne watuhumiwa namba mbili hadi tisa
wanatuhumiwa kwa kosa la kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria namba
86(1)(2)(b) cha uhuwifadhi wa wanyama pori sheria No 5/2009 sambamba na sura ya
14(d) na sura 57(1) cha uhujumu uchumi sura ya 200.
Katika maelezo ya kosa hilo ilidaiwa mahakamani hapo kuwa
washtakiwa kati ya 29/01/2016 na tarehe 6/02/2016 katika wilaya ya meatu mkoa
wa simiyu walikamatwa na nyara za serikali ambazo ni meno ya tembo yenye uzito
wa kilo 31 yenye thamani Milioni 32,891,100 bila ya kibali cha serikali.
Katika shtaka namba tano watuhumiwa namba moja na mbili
ambao ni Iddy Mashaka (49) pamoja na Shija Mjika (38) wanatuhumiwa na uuzaji wa
nyara za serikali kinyume na kifungu cha sheria 84(1) cha uhuwifadhi wa wanyama
pori sheria No 5/2009 sambamba na sura ya 14(b) na sura 57(1) cha uhujumu
uchumi sura ya 200.
|
Katika kosa hilo wakili alisema kuwa kati ya tarehe
6/01/2016 na tarehe 1/02/2016 katika wilaya a Meatu Mkoani Simiyu, watuhumiwa
walikamatwa wakiwa wanajihusisha na uuzaji wa nyara za serikali bila ya kibali.
Hata hivyo katika kesi namba mbili ya Mauaji wakili Mlekano
aliiambia mahakama kuwa watuhumiwa ambao ni Shija Mjika (38), Njile Gunga (28)
Dotto Pangali ( 42) pamoja na Moses Mandago (28) wanashtakiwa kwa kosa la
mauaji kinyume che sheria ya 196 na 197 cha kanuni ya adhabu namba 16
iliyofanyiwa mwaka 2002.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao mnamo tarehe
29/01/2016 katika hifadhi ya Mwiba kijiji cha Makao wilaya ya Meatu Mkoani
Simiyu walimuua rubani wa ndege aina ya helkopta rubani wake Rodgers Gower (37)
raia wa uingereza.
Katika kesi zote Mbili kwa mujibu wa hakimu huyo alisema
kuwa watuhumiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa
na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, ambapo keshi hizo zilihairishwa mpaka terehe
24/02/2016 mpaka zitakapotajwa tena.
|
Sambamba na hayo katika kesi ya tatu ambayo ni kukutwa na
siraha kinyume cha sheria na pasipo leseni ilisikilizwa katika mahakama hiyo
chini ya Hakimu mfawidhi wa wilaya Bariadi Mary Mrio ambapo watuhumiwa
walikabiliwa na mashitaka matano
Watuhumiwa hao ni Mange Buluma,Shija Mjika,Dotto
PanganiNjile Ngunga,Moses Mandagu,Dotto Huya na Mwigulu Kanga ambapo baadhi yao walikiri kumiliki siraha
kinyume cha sheria pamoja na riasi akiwemo njile aliyetungua helkopta hiyo.
|
Watuhumiwa hao ambao Shija Mjika, Moses Mandagu, Njile
Ngunga pamoja na Dotto Pangani walikiri mashtaka mawili ambayo ni kukutwa na
siraha aina ya bunduki Riffle 303 Namba 06490 kinyume cha sheria pamoja na
risasi mbili.
Hata hivyo Njile Ngunga pamoja na Moses Mandagu walikiri pia
katika shtaka la tatu, nne pamoja na tano la kukutwa na siraha bila ya kibali,
kumiliki risasi bila ya kibali, pamoja na kumiliki tena risasi kinyume cha
sheria huku wengine kati ya hao wakikana makosa hayo.
Hata hivyo mahakama haikuweza kutoa hukumu juu ya watuhumiwa
hao waliokiri kutokana na vielelezo kutokuwepo mahakamani hapo, ambapo kesi
hiyo ilihairishwa mpaka kesho (Leo).
Watuhumiwa wote walirudishwa rumande.
|
No comments:
Post a Comment