Pages

Saturday, February 20, 2016

TAZAMA PICHA:::YANGA WAINYONYOA SIMBA KWA GOLI 2 BILA

 Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akienda chini katika harakati za kuwania mpira na benki wa Simba, Abdi Banda katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0.
 Beki wa Simba, Mohamed Hussein akimtoka mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke.
 Mshambuliaji wa Simba, Amis Kiiza akimfariji beki wa timu hiyo, Abdi Banda baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo kati ya Sima na Yanga, Jonesia Rukyaa. 
 Baadhi ya watoa huduma ya kwanza kwenye uwanja wa Taifa wakati wa pambano la Simba na Yanga wakielekea kutoa msaada wa kwanza kwa mmoja wa mashabiki wa Yanga aliyepoteza fahamu.

 
 Beki wa Yanga, Mwinyi Haji akimiliki mpira huku akizogwa na Mwinyi Kazimoto.
 Mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wa timu yao.
 Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma (katikati) akisdhangilia bao lake aliloifungia timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara  dhidi ya Simba.
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akimtoka kipa wa Simba, Vicent Angban na kuipatia timu yake bao la kwanza katioka mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.Chanzo Fransis Dande

No comments:

Post a Comment