Hatimaye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba na mdogo wake Mwamvita Makamba wamejibu tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa raia wa Italia, Vincenzo Cozzolino ili wamsaidie kupata zabuni ya ujenzi kupata ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.
Hata hivyo, Cozzolino ambaye alianza kwa kuwashutumu ndugu hao, amekanusha tena kwa barua inayoeleza kuwa alifanya hivyo kwasababu ya kutaka kulipiza kisasi kwa Mwamvita kutokana na masuala yao binafsi na Mwamvita aliyekuwa mpenzi wake.
Issue ni complicated kidogo lakini kwakuwa wote kwa vinywa vyao wamelijibu sakata hili, tuangalie walichosema.
JANUARY MAKAMBA
January amepigiwa simu na mwandishi aitwaye Adam na amemueleza kuwa Cozzolino alikuwa mpenzi wa dada yake na wakati wakiwa pamoja alikuwa akimsumbua sana Mwamvita amkutanishe naye.
Anasema dada yake aliendelea na uhusiano na Cozzolino lakini baadaye akashangaa kuona kwamba dada yake hamzungumzii tena.
Mwamvita alimueleza kuwa waligombana baada ya kugundua kuwa mtu huyo alikuwa naye kwa lengo la kumtaka amuunganishe na viongozi wa nchi. Aligundua kuwa uhusiano huo ulikuwa wa kutumiwa zaidi.
Pia anasema mtu huyo alimuomba Mwamvita amkutanishe na katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi. Pia waligombana kuhusiana na biashara ya kutengeneza kahawa kwenye maofisi ambapo walitakiwa kila mmoja awekeze dola 50,000. Mwamvita alikuwa na mashaka na biashara hiyo hivyo aliwekeza nusu tu ambayo ni 25,000.
Bahati mbaya biashara hiyo ilikufa na ndipo Mwamvita alipata uhamisho kwenda Afrika Kusini.
Anasema Cozzolino alianza kudai apewe na Mwamvita $25,000 iliyokuwa imesalia kwenye mtaji wa uwekezaji huo. Hivi karibuni ndipo alipotaka tena aonane na January kwaajili ya kutoa malalamiko yake hayo.
January anasema dada yake alimuambia ana mpango wa kuuza kiwanja chake ili amlipe Cozzolino fedha yake baada ya kuchoshwa na usumbufu wake. Anasema alikuja kugundua kuwa alianza kurekodi kila mazungumzo waliyokuwa wakifanya na hivi karibuni akaanza kumtishia kuwa atayasambaza mtandaoni kitu ambacho amekifanya hivi karibuni.
January amesema alifuatilia na kugundua kuwa Cozzolino alijiingiza kwenye matumizi ya unga na alifukuzwa alipokuwa akiishi na kuamua kuishi Hyatt Hotel ambapo napo amezuiwa kutoka kutokana na madeni anayodaiwa.
Amesema kuwa wakati anatengeneza website yake ya Bumbuli alimuomba dada yake amchangie na kwamba huenda naye alitoa chochote na hivyo naye kuingizwa kwenye mgogoro wao. January amesema angeona ni jambo la msingi kama mtu huyo angeenda kushtaki jambo hilo mahakamani na sio kuweka vitu binafsi kwenye mtandao.
MWAMVITA
Anasema alikutana na Cozzolino mwaka 2011, anafanya kazi ya udalali na walikuwa na uhusiano wa kimapenzi ambao anadai ni wa muda mfupi sana.
“Sikujua kama alikuwa dalali tapeli, alikuwa anataka tu kunitumia mimi kujuana na watu kujua hapa na pale,” anasema Mwamvita.
“Ndiyo maana sikumtambulisha. Haya mambo ni ya kwake mwenyewe, unajua yule mtu anatapatapa, anatafuta kiki. Hii yote ni maneno ya mtu ambaye ni mkosaji, hakuna chochote, 2010 halafu baadaye unaanza kumrekodi mtu unazungumza yeye kumlead kuona kwamba amekosea mambo gani. Hakuna lolote katika hili suala, January hahusiki kabisa. Huku ni kutafuta tu kiki na kumhusisha mtu ambaye hayupo,” ameongeza.
Amesema alimtambulisha kwa watu wachache ambao wote aligombana nao na kuwatapeli na kwamba sasa hivi ameyumba kiuchumi. “Nashangaa wanaobeba hili suala na kuweka mtandaoni hawajui undani wake.”
COZZOLINO
— Vincenzo Cozzolino (@vhtltd) March 6, 2016
Ameamua kukanusha maneno yote aliyosema mwanzo na kuandika:
Jina langu ni Vincenzo Cozzolino. Katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita kumewepo na mkanganyiko mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uhusika wangu kwenye familia ya Makamba. Hakuna aliyesikia kutoka kwangu hivyo nataka kuweka vitu sawa. Nimemfahamu Mwamvita Makamba binafsi kama rafiki yangu kuanzia mwaka 2009. Mwaka 2011 uhusiano wetu ulikuwa wa karibu zaidi.
Nilijua kuhusu kaka yake, hatimaye watu wanapokuwa na uhusiano wa karibu jinsi ambavyo uhusiano wangu na Mwamvita ulikuwa, inaeleweka vizuri kuwa nilifahamiana na kaka yake pia. Sikumuomba afanye chochote kwaajili yangu. Sikuwahi kumuomba anisaidie kwenye mambo yangu ya biashara. Sikuwahi kumpa fedha. Siku chache nilizokutana naye zilikuwa za matukio ya kijamii. Nilikuwa na matatizo na Mwamvita. Uhusiano wetu ulikuwa mzuri mwanzoni lakini ukaharibika mwishoni. (Kama wanavyosema, usiingize biashara kwenye maisha binafsi) uhusiano wetu haukumhusisha kaka yake kabisa.
Mimi na Mwamvita tulikuwa na migogoro binafsi. Nilichukia pindi alipochelewa kukamilisha masuala ya muhimu. Nilitaka kuweka wazi hisia zangu kwenye umma, bila kufikiria madhara yatakayojitokeza kwa heshima ya Mheshimiwa January Makamba, hili ni suala binafsi kati yangu na Mwamvita Makamba. Nilirekodi na kusambaza mazungumzo ya faragha (kulipiza kisasi).
Nataka kuomba radhi kwa Mheshimiwa Mzee Yusuf Makamba na familia yake (na January) kwa kuwaingia kwenye mgogoro wetu na maisha binafsi. Mimi si mhalifu. Nilikuja kwenye nchi hii (miaka 1991, hakuna rekodi ya mimi kuwa mhalifu).. kwasababu naipenda pamoja na watu wake na niliona ningeweza kuwa na maisha hapa. Kitu ambacho nilifanya kwa miaka mingi hadi leo.
No comments:
Post a Comment