Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na watumishi waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Abaas Kandoro Machi 17 mwaka huu . |
Mkuu wa Mkoa Mstaafu Abbas Kandoro akizungumza na watumishi na baadhi ya viongozi (hawapo pichani)waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofsini na Mkuu wa Mkoa mpya Amosi Makalla Machi 17 mwaka huu. |
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya wakiwa makini kumsikiliza Mkuu wa Mkoa mstaafu Abbas Kandoro wakati awaaga rasmi mara baada ya kustaafu rasmi nafasi hiyo. |
Na Emanuel Madafa,
Mbeya.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya,
Amos Makala, amewaagiza watendaji wote
wenye dhamana ya kulinda afya na usalama wa wananchi kuhakikisha kuwa ugonjwa
wa kipindipindu unakuwa historia mkoani Mbeya kwa kusimamia usafi katika ngazi
zote za kijamii.
Mbali na agizo hilo ,
pia Makala amewaagiza Wakuu wote wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani
humo kuandaa madawati ya malalamiko katika kila siku za Alhamisi kuanzia ili kusikiliza malalamiko ya wananchi
kuhusu kero mbalimbali zinazojitokeza kwenye maeneo yao.
Mkuu huyo mpya wa Mkoa
wa Mbeya ametoa maagizo hayo katika
hafla fupi ya kukabidhiwa ofisi ya mkoa wa Mbeya na mtangulizi wake, Abbas
kandoro, ambaye amestaafu utumishi wa umma baada ya kufanya kazi kwa miaka 40
kuanzia mwaka 1976.
Amesema suala la ugonjwa
kipindupindu hatopenda kulisikia katika uongozi wake hivyo amezitaka mamlaka
husika kuwajibika ipasavyo ili kudhibiti kabisa ugonjwa huo hatari.
Wakati huo Makala amepiga
marufuku matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watumishi wa umma mkoani humo,
wakati wa saa za kazi ili kutoa fursa kwa watumishi hao kutimiza vyema majukumu
yao kazini.
Ameonya kuwa hatamvumilia mtumishi yeyote atakayebainika
kupoteza muda mwingi kwenye mitandao hiyo huku akishindwa kutimiza majukumu
yake katika kuwatumikia wananchi.
Hata hivyo, Makala
alitahadharisha kuwa haitaji majungu ya aina yoyote kutoka kwa watumishi wa
sekta wala wanannchi mbalimbali mkoani hapa ili kuhakikisha kuwa kila mtu
anatimiza majukumu yake na si kukwamishana katika utendaji wa kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa
Mkoa Mstaafu Abaas Kandoro amewashukuru watumishi na viongozi mbalimbali kwa
ushirikiano waliompa wakati wa utumishi wake na kuahidi kutoa ushirikiano kwa
mkuu wa mkoa huo Amosi Makala .
No comments:
Post a Comment