Pages

Wednesday, March 16, 2016

POLISI ARUSHA WAUWA MAJAMBAZI WAWILI NA KUKAMATA BUNDUKI



Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa na jeshi laPolisi mkoa wa Arusha baada ya kurushiana risasi wakitaka kuiba fedha kwenye kituo cha utafiti wa kilimo cha  AVRDC wilaya ya Arumeru majira ya saa tano za usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amesema baada ya Polisi kupata taarifa  ya mbinu hizo waliweka mtego na baadae watu wanne walitokea kwenye eneo hilo walipo waona askari wakaanza kuwarushia risasi kisha polisi wakajibu mapigo.


Kamanda Sabasi amesema katika tukio hilo pia wamefakikiwa kukamata bunduki mbili aina ya Shotgan Pump na ya kawaida moja kati ya hizo inadaiwa  iliibiwa kwenye kituo cha afya tumaini kinacho milikiwa na masista wa RC mwezi wa pili mwaka huu na kwamba majambazi wengine wawili walifanikiwa kukimbia.

CHANZO: ITV TANZANIA

No comments:

Post a Comment