![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhKJ9PruEJaHdhqGeYE1U05nfWtpVZ74LByULeGLeaXPkFiWr4rpk69gBbU69uftjYq5bUMnLajB8u96qNfDBn5ANlVtUPpEY-KW6GRQKMc9tWzA-kfqBw7JNPidisMozgb1Dxm0GKMvnc/s280/sukari2.jpg)
Siku chache baada ya Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kutangaza zuio la uingizwaji wa bidhaa ya sukari kutoka nje ya nchi,
leo March 8 2016 Serikali kupitia bodi ya sukari Tanzania, imetangaza viwango
vipya vya bei ya sukari nchini vitakavyoanza kutumika hivi karibuni, akiongea
na waandishi wa habari Mkurugenzi wa bodi ya sukari Tanzania Henry Semwanza
amesema.
Serikali, kupitia bodi ya Sukari Tanzania, inawaarifu
wananchi wote kuwa bei ya rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo
moja‘
‘wafanyabiashara wote wanapaswa kuzingatia agizo hili,
pamoja na kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi
bila kuihodhi‘
‘Maafisa biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na
kusimamia utekelezaji wa agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na hawatasita
kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale watakaobainika kupandisha bei ya
bidhaa hiyo‘
No comments:
Post a Comment