Picha za ujio wa Makatarsi na huyo anayeonekana hapo ni Mkurugenzi wa ZEC Salim Kassim Ali akitoa maelezo ya kuwasili kwake uwanja wa ndege Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imendelea na msimamo wake wa
kuhakikisha kwamba vyama vyote vinashiriki katika uchaguzi wa marejeo
unatarajiwa kufanyika march 20 mwaka huu.
Hayo yamedhihirikia leo pale ZEC waliupopokea
makaratasi ya kupigia kura kutoka Afrika ya Kusini yakiwa yamechapishwa
ikihusisha wagombea woote hata wale ambao waliomba kuondolewa katika karatasi
hizo kwa madai kwamba uchaguzi huo si halali.
Akizungumza na waandishi baada ya kupokea karatasi hizo Mkurugenzi
wa Tume hiyo Salim Kassim Ali aliweza kuonesha mfano wa karatasi hizo ambazo
hata Chama kikuu cha Upizani CUF kilichopiga kelele mara kwa mara nacho
kimeorodheshwa .
“Wagombea ni walewale waliokuwa katika uchaguzi uliopita ambao
waliteuliwa tarehe 6 september 2015 na kama mnavyoona karatasi zetu za mfano”
alisema Ali.
Alisema kujiondoa kuna taratibu za kisheria ambazo hazikufuatwa
kuda kutokana na hilo wamefanya uchapishaji ule ule wa mwaka jana.
Alisema kilichobakia sasa karatasi hizo ni kuzipeleka kwenye ghala
la kuhifadhia karatasi hizo hadi hapo Tarehe 17/03/2016 ambapo zitaaza
kusambazwa katika vituo.
Alisema tarehe 18 mwezi huu wataaza kuzipeleka kisiwa cha Pemba na
19 ni katika vituo vyote vya Unguja.
Ali alieleza kwamba wamechapisha makaratasi hayo kulingana na Idadi
ya wapiga kura wote ambao wameorodheshwa katika Daftar la wapiga kura Zanzibar
ambao ni 503850.
“Tutahakisha mara hii karatasi zoote zimefika mapemaa sanaa ili
kuondoa matatizo ambayo yailiweza kujitokeza katika chaguzi zilizopita” alisema
Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wa gharama za uchapishaji na usafiri muhasibu wa ZEC
Yusouf Ali Hassan alisema mara hii wametumia Ud250000 kiasi ambacho ni
kidoogo kulingana uchaguzi uliopita kwa tofauti ya Dola 50000.
Alifahamisha kwamba ghara zote hizo ziliweza kutolewa na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar bila ya mkopo wowote.
“Tulilipa kwa awamu 60% na ilipokamilika kazi ya uchapisha
tumemaliza kilichabakia na kwa maana hiyo hatudaiwi” alisema Hassan.
Akizungumza kiwanjani hapo mwakilishi wa chama cha TADEA Rashid
Mchenga alisema anaishukuru ZEC kwa kufanya mambo yao kwa wakati. Alisema
wao watashiriki kifua mbelee na hana wasiwasi katika uchagfuzi huo.
Ikumbukwe kwamba vyama zaidi ya 10 viliaandikia ZEC vikiomba
kuondolewa katika katasi hizo lakini mambo yamekwenda kinyume chake na sasa
majinan na picha yataonekana vile vile.
Vyama vyoote 14 ambavyo vilishiriki uchaguzi 25 October 2015 ndivyo
vile vile ambavyo vimechapishiwa makaratasi ya kupigia kura.
Vyama ambavyo vitashiriki ni ACT Wazalendo, ADA-TADEA, ADC, CCK,
CCM, CHAUMA, CUF, DP, JAHAZI ASILIA, MAKINI, SAU na TLP.
No comments:
Post a Comment