Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wajumbe wa baraza
hilo wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza
Ajali za Barabarani. Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza ambaye pia ni
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.Kikao hicho
kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa
la Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha
Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akifungua kikao cha kujadili
maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani.Kushoto ni
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongoza kikao cha kujadili
maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani. Kushoto ni
Katibu Mtendaji wa baraza ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini, Mohamed Mpinga.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi
wa wizara hiyo, Dar es Salaam.(
Mjumbe wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu
Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Mossi Ndozero, akiwasilisha taarifa ya
maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani kwa Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo
pichani), wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya mkakati huo,
kilichofanyika katika ukumbi wa wizara, Dar es Salaam.
Mjumbe wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani, Hamza Kasongo(kulia), akichangia mada wakati wa
kujadili taarifa ya maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za
Barabarani wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya mkakati huo.Kushoto
ni mjumbe wa baraza hilo Henry Bantu. Kikao hicho kilifanyika katika
ukumbi wa wizara, Dar es Salaam.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment