Pages

Sunday, October 16, 2016

SALAMU ZA RAMBIRAMBI CCM, KIFO CHA DKT MASABURI NA MZEE MGODA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Abdulrahman Kinana ameitumia salamu za rambirambi familia ya Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Iringa Mzee Tasili Mung’wenya Mgoda aliyefariki dunia jana tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Hospitali ya Wilaya ya Mafinga.

Mzee Mgoda amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya TANU baadae CCM na Serikalini ambapo amekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Mafinga, Katibu wa CCM ngazi ya Wilaya na Mkuu wa Wilaya Mstaafu.


Katika Salamu hizo Ndg Kinana amesema amepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa kifo cha Mzee Tasili Mgoda ambaye alikuwa ni sehemu ya hazina ya wazee wa CCM na kwamba anaungana na familia ya marehemu, ndugu na jamaa katika kipindi hiki kigumu cha huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao.

WanaCCM tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Mzee Tasili Mung’wenya Mgoda.  Amina

Imetolewa na:-
 
SELEMAN Y. MWENDA
Kny: MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
15/10/2016

No comments:

Post a Comment