Tanga,
MWENYEKITI wa mtaa wa Centrol Tanga, Diana Mussa, amewataka wakazi wa
eneo hilo kuweka mazingira ya usafi kwa kila nyumba ili kuondosha
kitisho cha magonjwa ya miripuko na kusema kuwa ambaye atakaidi agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa duka la kuuza umeme la Zola
lililopo barabara ya Markert Street Tanga juzi , Diana amesema agizo
hilo litakuwa endelevu na ofisi yake ikiongozwa na yeye kila siku
asubuhi atafanya ukaguzi kwa kila mtaa.
Amesema
halmashauri ya jiji imeweka vyombo maalumu vya kuhifadhia takataka na
magari ya kusomba taka mtaani hivyo kutaka kila mmoja kuhakikisha eneo
lake linakuwa katika mazingira mazuri.
Akizungumza
kwenye ufunguzi huo,Meneja mauzo kanda ya Kaskazini Tanga na
Kilimanjaro, Peter Laizer, amewataka wajasiriamali wadogowadogo kutumia umeme wa Zola na kusema kuwa ni wa gharama nafuu.
Amesema
Wajasiriamali wa mbogamboga na matunda wanaweza kuinua kipato chao kwa
kusindika na kuweza kusafirisha kwenda katika masoko ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki ambako watajitangaza tofauti na kutegemea mteja mmoja mmoja.
Amesema
umeme huo ni mkombozi kwa watu wa kipato chote, cha chini, kati na juu
na, umeme huo utaondolea adha mbalimbali kama za kuchaji simu mbali na
nyumbani na ufuatiliaji wa taarifa katika Luninga pamoja na kusaidia
watoto kusoma katika mwanga bora nyakati za usiku.
“Umeme
huu ni mkombozi kwa wananchi wa Tanga kwani ni rahisi, hauchukui muda
kuupata na pia utawasaidia wananchi kuhifadhi kiasi cha pesa ambacho
walikuwa wanakitumia kwa nishati nyingine kupata mwanga, Pia humsaidia
mwananchi wa kipato cha chini kubadilisha maisha kwa kupata habari,
taarifa pamoja na burudani, kwani mbali na taa na kuchaji simu pia
utapata Radio na TV za sola”alisema Laizer
Alisema
umeme huo umekuwa mkombozi kwa wanafunzi wa vijijini ambao walikuwa
hawana uwezo wa kujisomea usiku au husoma katika mwanga hafifu wa
vibatari sasa wanapata mwanga salama kwa afya ya mwili na macho.
Mwisho
Mwenyekiti wa mtaa wa Centrol Tanga, Diana Mussa, katikati akikata uzi kuashiria ufunguzi wa dula la kuuza umeme wa Zola Markert Street mjini Tanga juzi , kushoto ni Msimamizi wa maduka ya Zola , Bethany Katen na kulia ni Mtendaji kata ya Centrol Bhati Marungu.
Meneja Mauzo kanda ya Kaskazini maduka ya kuuza umeme wa Zola , Pitter Laizer akitoa maelezo ya matumizi wa umeme wa Zola wakati wa ufunguzi wa duka hilo juzi.
Wakazi wa Tanga wakiangalia radio za kuchaji baada ya kuchajiwa kwa kutumia umeme wa Zola wakati wa ufunguzi wa duka la kuuzia umeme wa Mypower Tanga juzi
Habari hii ni kwa hisani ya blog ya kijamii ya tangakumekucha 0655 902929
No comments:
Post a Comment