Pages

Saturday, February 1, 2014

MWENYEKITI WA CCM,RAIS JAKAYA KIKWETE AWASILI JIJINI MBEYA JIONI YA LEO TAYARI KWA KUONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM KESHO.

 Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwapungia Viongozi mbalimbali wa chama,Serikali,na viongozi wa dini na watu mbalimbali (hawapo pichani) waliofika kumpokea mara baada kuwasili jioni ya leo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe  tayari kwa kuongoza maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya chama hicho yatakayofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine mjini humo. 
 Pichani Kati ni Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa chama hicho,Ndugu Kinana (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh Godfrey Zambi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe jioni ya leo. 
Pichani kati Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete pamoja na Viongozi wa ngaji za juu wa chama hicho,kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho,Ndugu Kinana,Makamu Mwenyekiti Taifa,Mh.Phillip Mangulla na shoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh Godfrey Zambi wakiwa kwenye kikao cha wanachana mbalimbali wa chama hicho (hawapo pichani) ndani ya ofisi ya makao makuu jijini Mbeya jioni ya leo mara baada ya kuwasili.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akilakiwa na waendesha boda boda kutoka sehemu mbali mbali,alipowasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa Songwe,jijini Mbeya mapema leo wakati alipokwenda kumpokea Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete aliyewasili jioni ya leo kwa ajili ya kuhserehekea maadhimisho ya miaka 37 ya chama cha CCM yatakayofanyika katika uwanja wa Sokoini mkoani humo.
 Katibu wa Uchumi na Fedha Bi.Zakia Meghji akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum na Mbunge wa jimbo la Rungwe Mashariki,Mh.Prof.Mark Mwandosya walipokutana jioni ya leo kwenye uwanja wa Ndege wa songwe walipokuwa wakimsubiri Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete aliyewasili leo jioni tayari kwa kuongoza maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya chama hicho yatakayofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine mjini humo. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kushoto akizungumza jambo kwa msisitizo na Waziri wa uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe,ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kyela walipokutana jioni ya leo kwenye uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Songwe walipokuwa wakimsubiri Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete aliyewasili leo jioni tayari kwa kuongoza maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya chama hicho yatakayofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine mjini humo. PICHA NA JIACHIE BLOG NA FULL SHANGWE  BLOG
8Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr.Jakaya Kikwete akivishwa skafu na vijana wa chipukizi mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili mkoani humo kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 10Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa serikali na chama. 11Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na  viongozi na wabunge 12Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na vijana wa UVCCM. 13 14Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwa katika kikao cha ndani na viongozi wa CCM mkoa wa Mbeya kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mzee Philip Mangula Makamu Mwenyekiti Bara na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi 15wajumbe wa harmashauri kuu mkoa wa Mbeya wakiwa katika kikao hicho.16Mary Mwanjelwa Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Mbeya akisalimiana na makada wa chama hicho kushoto ni Kada wa CCM Richard Kasesela. 17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh. Dr. Norman Sigalla wakati aliookuwa akizungumza jambo naye katikati ni Kada wa CCM Bw. Mwakipesile na kuliani Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abas Kandoro. 18 19Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Kamnda wa polisi mkoa wa Mbeya SACP  AHMED Z. MSANGI wakati wa mapokezi hayo. 20Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na viongozi wanawake wa mkoa wa Mbeya. 21Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza kwa msisitizo  na Dr. Harrison Mwakyembe Waziri wa Uchukuzi wakati wa mapokezi hayo. 22Ndege ya Rais Jakaya Kikwete ikiwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya

No comments:

Post a Comment