Manchester
City imeizaba Manchester United 6-1 kwenye uwanja wa Old Trafford.
Kinyume na matarajio ya
Wengi, Man United walishindwa kabisa kuhimili vishindo vya majirani
zao na mahasimu wao wa jadi. Hadi mapumziko City walikuwa wakiongoza
kwa goli moja lililofungwa na Mario Balotelli.
Man
United walicheza karibu kipindi chote cha pili wakiwa na mchezaji mmoja
pungufu baada ya beki Jonny Evans kupewa kadi nyekundu kwa kumzuia
Balotelli kwenda kumuona kipa wa United David De Gea.
Baada ya
kutolewa kwa Evans, karamu ya magoli ilianza kwa City. Balotelli
aliongeza bao la pili katika dakika ya 60. Sergio Aguero akafunga bao
la tatu katika dakika ya 69. Edin Dzeko baada ya kuingia kama mchezaji
wa akiba alifunga bao la nne katika dakika ya 90, David Silva bao la
tano na Dzeko tena kupiga msumari wa mwisho katika filimbi ya mwisho ya
mchezo.
Bao
pekee la kufutia machozi la United lilifungwa na Darren Fletcher katika
dakika ya 81.
Matokeo haya yanaipa City pointi tatu ambazo zinaifanya
kuendelea kuongoza kwa pointi tano zaidi ya United.
Katika
michezo mingine, Arsenal iliizaba Stoke City 3-1. Gervino aliandika bao
la kwanza katika dakika ya 27, ingawa bao hilo lilisawazishwa na Peter
Crouch. Hata hivyo Robin Van Persie ambaye alianza bechi katikika
mchezo huo aliingia na kufunga mabao mawili.
Everton
nayo ikicheza ugenini ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham.
Mabao ya Everton yakifungwa na Royston Drenthe, Luis Saha na Jack
Rodwell. Bao la Fulham lilifungwa na Bryan Ruiz.
No comments:
Post a Comment