Mwishoni mwa wiki kulifanyika UN Family Day katika viwanja vya Leaders Club wakati wa Shamrashamra za wiki ya maadhimidho ya 66 ya Umoja Mataifa nchini ambapo ilipigwa mechi kati ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa (White Jersey) na wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (Blue Jersey) ambapo timu ya Wizara ya Mambo ya Nje iliibuka kidedea baada ya kuichapa timu ya UN bao 4-2.
Kapteni wa timu ya Mpira wa Miguu ya Umoja wa
Mataifa akipokea kikombe cha ushindi wakati wa mchezo wa kuvuta kamba
kwa niaba ya wafanyakazi wenzake kutoka kwa mgeni rasmi Mkuu
wa Itifika Balozi A. Itatiro. Chini UN Oyeee....
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa katika picha ya pamoja na kikombe chao.
Vikombe kwa ajili ya
washindi wa mechi kati ya UN na Wizara ya Mambo ya Nje.
Ililfika zamu ya Wakubwa kupimana nguvu katika
mchezo wa kuvuta kamba baina ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa na Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.
Wazazi wakionekana kufurahi na watoto wao katika
mkusanyiko huo uliokutanisha Familia za Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa
na wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kucheza
pamoja, kula pamoja, kunywa pamoja na kushiriki michezo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment