Pages

Sunday, October 23, 2011

Mashindano ya baiskeli Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge yarindima jijini Mwanza

 
Hatimaye Richard Laizer wa mkoani wa Arusha ndiye ametegua kitendawili cha nani anayepaswa kuwa mshindi wa mbio za wazi za baiskeli za Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge baada ya kuwashinda washiriki wengine zaidi ya 400 walijitokeza kushiriki kwenye mashindano hayo kwa upande wa wanaume.
Hapa mshindi huyo wa mbio za Mwanza Open Vodacom Cycle Challenge 2011 kutoka klabu ya Arusha Cycling Richard Laizer akipokea zawadi yake ya shilingi milioni 1.500.000 kutoka kwa Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya Vodacom Tanzania George Rwehumbiza mara baada ya kutajwa katika mbio hizo za kilomita 196 zilizoanzia Busanda mkoani Shinyanga na kumalizikia Bugando Hills jijini Mwanza.
Mbio hizo ziligawanyika katika makundi matatu ambapo kulikwa na wanawake wenye ulemavu ambao waliendesha baiskeli kilomita 10 wakati wanaume wenye ulemavu waliendesha umba;li wa kilomita 15.
Kwa upande mwingine kulikuwa na mbio za wanawake ambao waliendesha baiskeli kwa umbali wa kilomita 80 wakati wanaume wakiendesha kwa umbali wa kilomita 196 ambao ndiyo ulikuwa umali mrefu zaidi Katika Picha kulia ni Steven Kingu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa na kulia kwa George Rwehumbiza ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL. Mdhamini mkuu wa mashiundano hayo ni kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ikishirikiana na wadhamini wenza kampuni ya bia ya Aerengeti SBL na Kituo cha redio cha Clouds
 
Richard Laizer wa mkoani wa Arusha ndiye akionyesha zawadi zake mara baada ya kukabidhiwa rasmi jioni ya leo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
 

No comments:

Post a Comment