Pages

Sunday, October 23, 2011

Ndugu wa Mflame wa Saudi Arabia, Prince Sultan, amefariki.


Prince Sultan ambaye angeweza kurithi ufalme, alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 80, na amekuwa akitibiwa saratani nchini Marekani.
Prince Sultan alikuwa mtoto wa mwanzilishi wa taifa la Saudi Arabia, Ibn Saud, na ni baba mmoja na mfalme wa sasa, Abdullah, ambaye piya ana zaidi ya miaka 80.
Mwandishi wa BBC katika Mashariki ya Kati anasema inavoelekea mtoto mwengine mwanamume wa Ibn Saud, atatangazwa kuwa mrithi wa ufalme, pengine Prince Nayef.
Lakini naye piya anakaribia miaka 80.
Na mwandishi wetu anasema swala linaloulizwa ni lini ufalme wa Saudi Arabia utakabidhiwa kwa kizazi cha vijana zaidi.

No comments:

Post a Comment