Pages

Monday, October 17, 2011

Miss Tanzania 2011 na kipindi cha njia panda watoa msaada wodi maalum ya watoto muhimbili jijini Dar

 
Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akimtazama mtoto wake ambaye
ameamua"kumuadapti" na kumpachika jina lake la Salha.
Miss Tanzania 2011 Salha Esrael wakishirikiana na kipindi cha Njia Panda  wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo pampas,sabuni za maji,mashuka na vinginevyo ambavyo ni vitu muhimu kwa watoto wenye umri chini ya mwezi mmoja katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwenye Wodi ya Watoto namba 36 (Neonatal Ward).Pichani Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akiwakabidhi baadhi ya vitu Manesi wa wodi hiyo maalum ya watoto kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ya Muhimbili. Mlimbwende huyo,Salha kwa hivi sasa ameamua kujikita kwenye harakati za kutetea haki za watoto wachanga walio chini ya umri wa mwezi mmoja ambao kitaalamu wanaitwa Neonates, "watoto hawa wamekuwa wakisahauliwa kwa kiasi kikubwa,watu wanawakumbuka kuwasaidia watoto kuanzia miaka mitano na kuendelea,wanakimbilia kutoa vyandalua na mambo mengine,lakini ukweli ni kwamba kundi la watoto hawa limesahaulika mno,kwa hiyo kupitia Miss Tanzania 2011 tukishirikiana na kipindi cha Njia Panda tumetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo pampas,sabuni za maji,mashuka na vinginevyo ambavyo ni vitu muhimu kwa watoto hawa ambao wamekuwa wakisahaulika siku hadi siku",alisema Salha. Aidha Miss Tanzania 2011 Salha Esrael “amemuadapti” mtoto ambaye ni yatima mwenye umri wa chini ya mwezi mmoja na kumpa jina la Salha,mtoto huyo ambaye kwa sasa anaonakana kuendelea vyema kiafya alikutwa ametupwa vichakani na kuokotwa na wasamaria wema ambao walimfikisha haraka kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili,wodi ya watoto namba 36 (Neonatal Ward).Miss Tanzania 2011 Salha amebainisha wazi kuwa atahakikisha anamlea mtoto huyo katika maisha yake yote. Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya kuvikabidhi vifaa hivyo mapema leo jioni kwa manesi wa wodi hiyo,Salha alisema kuwa yeye atajikita zaidi katika kutetea haki za watoto hao wachanga ambao wamekuwa wakisahaulika kwa asilimia kubwa,ilhali watoto wengi wanaanzia kwenye hatua hiyo, “huu ni mwanzo tu wa kampeni hii,lakini nitakaporudi kwenye mashindano ya Miss Word yanayotarajiwa kufanyika hapo baadaye mwaka huu,mimi pamoja na wadau wengine tutahakikisha tunafanya kampeni kubwa ya kuihamasisha na kuielimisha jamii katika suala zima la kuwasaidia watoto hawa,ambao baadhi yao hutelekezwa na wazazi wao kutokana na kuwa na matatizo mbalimbali wangali wachanga”, Salha akiwa amembeba mmoja wa watoto yatima aliyezaliwa chini ya umri wa mwezi mmoja na Mama yake kufariki na kuhifadhiwa kwenye chumba maalum cha kuhifadhia watoto hao. Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akifafanua jambo kuhusiana na misaada waliotoa leo jioni kwa wodi ya watoto wanaozaliwa chini ya umri wa mwezi mmoja wakishirikiana na kipindi cha Njia Panda. Mkuu wa Itifaki ya Miss Tanzania 2011,Albert Makoye akiushukuru uongozi wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwapa sapoti ya kutosha kwa kile ambacho wamedhamiria kukifanya kwa ajili ya kuwasaidia watoto wachanga wanaozaliwa wakiwa chini ya umri wa mwezi mmoja,kuhakikisha wanawaisaida kwa kila hali na pia kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na suala zima la watoto hao,ambao baadhi yao wazazi wao wamekuwa wakiwatelekeza,ama hata kuwatupa kwenye mapipa ya taka,vicha na vinginevyo,wakati watoto hao wana haki zote za kuishi kama watoto wengine . Mwendeshaji wa kipindi cha Njia Panda ambao ndio waratibu wa zoezi zima la ushiriki wa Miss Tanzania kutoa msaada kwenye wodi hiyo maalum,Dr Isaac Maro akizungumza machache kuhusiana na tukio hilo,pichani kati ni Miss Tanzania 2011,Salha Esrael pamoja na mdau Simalenga kutoka Clouds FM akirekodi taarifa muhimu za tukio hilo. Dr Sebastian Ndege ambaye pia ni mratibu kutoka Kipindi cha Njia Panda akizungumza machache kuhusiana na tukio hilo adhimu kabisa,kulia kwake ni manesi wanaohudumia wodi hiyo maalum ya Watoto wenye umri chini ya mwezi mmoja.

No comments:

Post a Comment