Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akimtazama mtoto wake ambaye
ameamua"kumuadapti" na kumpachika jina lake la Salha.
Miss Tanzania 2011 Salha Esrael wakishirikiana na kipindi cha Njia
Panda wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo
pampas,sabuni za maji,mashuka na vinginevyo ambavyo ni vitu muhimu kwa
watoto wenye umri chini ya mwezi mmoja katika hospitali ya Taifa
Muhimbili kwenye Wodi ya Watoto namba 36 (Neonatal Ward).Pichani Miss
Tanzania 2011,Salha Esrael akiwakabidhi baadhi ya vitu Manesi wa wodi
hiyo maalum ya watoto kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ya Muhimbili.
Mlimbwende huyo,Salha kwa hivi sasa ameamua kujikita kwenye harakati
za kutetea haki za watoto wachanga walio chini ya umri wa mwezi mmoja
ambao kitaalamu wanaitwa Neonates, "watoto hawa wamekuwa wakisahauliwa
kwa kiasi kikubwa,watu wanawakumbuka kuwasaidia watoto kuanzia miaka
mitano na kuendelea,wanakimbilia kutoa vyandalua na mambo
mengine,lakini ukweli ni kwamba kundi la watoto hawa limesahaulika
mno,kwa hiyo kupitia Miss Tanzania 2011 tukishirikiana na kipindi cha
Njia Panda tumetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo pampas,sabuni za
maji,mashuka na vinginevyo ambavyo ni vitu muhimu kwa watoto hawa
ambao wamekuwa wakisahaulika siku hadi siku",alisema Salha.
Aidha Miss Tanzania 2011 Salha Esrael “amemuadapti” mtoto ambaye ni
yatima mwenye umri wa chini ya mwezi mmoja na kumpa jina la
Salha,mtoto huyo ambaye kwa sasa anaonakana kuendelea vyema kiafya
alikutwa ametupwa vichakani na kuokotwa na wasamaria wema ambao
walimfikisha haraka kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili,wodi ya
watoto namba 36 (Neonatal Ward).Miss Tanzania 2011 Salha amebainisha
wazi kuwa atahakikisha anamlea mtoto huyo katika maisha yake yote.
Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya kuvikabidhi vifaa hivyo mapema
leo jioni kwa manesi wa wodi hiyo,Salha alisema kuwa yeye atajikita
zaidi katika kutetea haki za watoto hao wachanga ambao wamekuwa
wakisahaulika kwa asilimia kubwa,ilhali watoto wengi wanaanzia kwenye
hatua hiyo, “huu ni mwanzo tu wa kampeni hii,lakini nitakaporudi
kwenye mashindano ya Miss Word yanayotarajiwa kufanyika hapo baadaye
mwaka huu,mimi pamoja na wadau wengine tutahakikisha tunafanya kampeni
kubwa ya kuihamasisha na kuielimisha jamii katika suala zima la
kuwasaidia watoto hawa,ambao baadhi yao hutelekezwa na wazazi wao
kutokana na kuwa na matatizo mbalimbali wangali wachanga”,
Salha akiwa amembeba mmoja wa watoto yatima aliyezaliwa chini ya umri
wa mwezi mmoja na Mama yake kufariki na kuhifadhiwa kwenye chumba
maalum cha kuhifadhia watoto hao.
Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akifafanua jambo kuhusiana na misaada
waliotoa leo jioni kwa wodi ya watoto wanaozaliwa chini ya umri wa
mwezi mmoja wakishirikiana na kipindi cha Njia Panda.
Mkuu wa Itifaki ya Miss Tanzania 2011,Albert Makoye akiushukuru
uongozi wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwapa sapoti ya
kutosha kwa kile ambacho wamedhamiria kukifanya kwa ajili ya
kuwasaidia watoto wachanga wanaozaliwa wakiwa chini ya umri wa mwezi
mmoja,kuhakikisha wanawaisaida kwa kila hali na pia kutoa elimu kwa
jamii kuhusiana na suala zima la watoto hao,ambao baadhi yao wazazi
wao wamekuwa wakiwatelekeza,ama hata kuwatupa kwenye mapipa ya
taka,vicha na vinginevyo,wakati watoto hao wana haki zote za kuishi
kama watoto wengine .
Mwendeshaji wa kipindi cha Njia Panda ambao ndio waratibu wa zoezi
zima la ushiriki wa Miss Tanzania kutoa msaada kwenye wodi hiyo
maalum,Dr Isaac Maro akizungumza machache kuhusiana na tukio
hilo,pichani kati ni Miss Tanzania 2011,Salha Esrael pamoja na mdau
Simalenga kutoka Clouds FM akirekodi taarifa muhimu za tukio hilo.
Dr Sebastian Ndege ambaye pia ni mratibu kutoka Kipindi cha Njia Panda
akizungumza machache kuhusiana na tukio hilo adhimu kabisa,kulia kwake
ni manesi wanaohudumia wodi hiyo maalum ya Watoto wenye umri chini ya
mwezi mmoja.
No comments:
Post a Comment