Pages

Sunday, October 23, 2011

Serikali ya mpito ya Libya imeiambia BBC kwamba maiti ya Kanali Gaddafi, itakabidhiwa kwa jamaa zake ama leo usiku au kesho, na kwamba maiti hiyo imeshakaguliwa.


Siku mbili baada ya kuuwawa, maiti ya Gaddafi imekuwa katika duka la nyama mjini Misrata, na imekuwa imeanza kuoza, huku wananchi wakipiga foleni kwenda kuitazama.
Kamanda wa wapiganaji wa serikali ya mpito ya Libya, waliomteka Muammar Gaddafi, anasema yeye anachukua dhamana kwa mauaji ya kiongozi huyo wa zamani, juzi, Alkhamisi.
Omran el Oweib, alisema Kanali Gaddafi ambaye alikuwa amejeruhiwa, alibururwa kutoka kwenye mtaro, ambamo alikuwa amejificha, alichukua hatua 10 tu na kisha alianguka chini.
Bwana el Oweib alisema haiwezi kujulikana nani alifyatua risasi iliyomuuwa.
Hapo awali, Shirika la kimataifa linalopigania haki za kibinaadamu, Amnesty International, lilitoa wito kwa Libya ijitahidi kutafuta ukweli kuhusu kifo chake, kwa sababu kila mmoja, pamoja na serikali ya mpito ya Libya, inasema kuwa inataka kuwa nchi itayoheshimu sheria, na haki za kibinaadamu ndio msingi wa mwanzo kuwekwa.
Maafisa wa daraja za juu wa serikali ya mpito wamesema sherehe rasmi itafanywa kesho, Jumapili, kutangaza kuwa Libya imeshakombolewa yote.
Waziri Mkuu Mahmoud Jibril alisema uchaguzi utafanywa katika miezi minane ijayo.
Alisema wapigaji kura watachagua baraza la taifa, litalotayarisha katiba mpya, ambayo itapigiwa kura ya maoni.

No comments:

Post a Comment