Kocha
Sam Timbe ambaye alifungashiwa virago na ‘Wanajangwani’ baada ya
kurejeshwa kwa kocha aliyemtangulia, Mserbia Kostadin Papic, ameutaka
uongozi wa klabu hiyo umlipe fedha zake ili aondoke zake nchini.
Akizungumza
jana na kwenye hoteli ya Markham, Timbe alisema kuwa anasikitishwa na
kile anachofanyiwa sasa na uongozi wa Yanga kwani aliamini kuwa
watatanguliza uungwana na kumlipa stahili zake mara tu walipoamua
kuvunja mkataba wake wa ajira.
"Ni
wao ndio walioamua kuvunja mkataba… wanapaswa kunilipa haki yangu ili
na mimi nifanye mambo mengine. Hadi sasa sijui ni lini watanilipa fedha
zangu," alisema Timbe.
Alisema
kuwa mbali na kuidai Yanga gharama ya kuvunja mkataba wake, pia anaidai
klabu hiyo fedha za kuingia mkataba wa kuifundisha timu hiyo pamoja na
mshahara wake wa mwezi uliopita hadi sasa.
"Niliposaini
mkataba mwezi Mei mwaka huu walinilipa sehemu tu ya fedha
tulizokubaliana na nyingine waliahidi kunilipa baadaye… lakini hadi
walipovunja mkataba Oktoba 23, hawakuwa wamenilipa fedha zilizobakia na
zote naamini kwamba watanilipa mara moja ili niondoke zangu,” alisema
Timbe, ambaye aliongeza kuwa hajui ni kwanini ametimuliwa ghafla wakati
timu aliyokuwa akiifundisha ilikuwa na mwelekeo mzuri na kukamata nafasi
ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya Bara.
"Baada
ya mechi yetu dhidi ya Oljoro, nilipewa barua ya kunijulisha kikao na
uongozi wa Yanga ili kujadili maboresho ya benchi la ufundi. Katika
barua hiyo niliambiwa kwamba kikao kitakuwa cha watu wanne ambao ni mimi
na viongozi watatu ambao wangefika hapa hotelini ninakoishi," alisema.
Hata
hivyo, Timbe anasema kuwa alishangaa kuona kuwa kesho yake anafuatwa na
kiongozi mmoja na kupewa barua ya kuvunja mkataba, bila kupewa maelezo
zaidi.
"Mimi
sikuwa na jinsi isipokuwa ni kudai haki yangu. Ila iliniuma moyoni
nilipokuja kufahamu kuwa tayari walishamleta kocha mwingine wa kutwaa
nafasi yangu. Jambo hili limenisikitisha sana," alisema Timbe.
No comments:
Post a Comment