Kuna kitu kinamsumbua Queiroz.
Amewasili
Ureno na bosi wake David Gill kufanya mazungumzo ya uhamisho wa winga
mpya kutoka kituo cha kukuza vipaji cha Sporting Lisbon, hivyo Queiroz
alikuwa anataka kuhakikishiwa kuwa United wanafanya uamuzi mzuri kwa
kulipa £17million kwa Luis Carlos Almeida da Cunha aka Nani.
“Carlos alikuwa hotelini in Lisbon,”
anakumbuka Pereira, mwenye umri wa miaka 64 na kiongozi wa jopo la
maskauti wa kuibua vipaji katika klabu ya Sporting ambaye ana heshima
kubwa nchini Ureno kwa kuvumbua vipaji vya nyota kama Luis Figo,
Cristiano Ronaldo, Paul Futre na Ricardo Quaresma.
Anaendelea Pereira, “Quieroz alikuwa anataka kujua kuhusu mentality ya Nani na kama angeweza kuhimili presha ya kuichezea United.
“Hakutaka
kujua kama alikuwa na miguu mizuri.Alijua kila kitu kuhusu hilo.Alitaka
kufahamu kuhusu tabia yake, vipi angeweza kukabiliana na mazingira ya
nchi mpya na timu mpya.
“Yalikuwa
majukumu mazito kwa Quieroz kwa sababu ulikuwa ni uhamisho wa Euro
million 25 na alitaka kuwa uhakika kwa 100%.Nilimtuliza na
kumuhakikishia alikuwa anamnunua mchezaji aliyekamilika.”
Masaa
kadhaa baadae United walikamilisha uhamisho wa kumsajili kijana wa
miaka 20 kwenda Old Trafford, na ukurasa mpya wa maisha ya Luis Nani
ukawa umefunguliwa.
Nani
alikulia katika mji wa Santa Filomena, mji mdogo uliojengwa katika
mteremko wa vilima vya Amadora kaskazini magharibi mwa jiji la Lisbon.
Asilimia
30 ya watu kwenye sehemu hiyo wenye umri kati ya miaka 15 na 30 wote
wana rekodi mbaya za uhalifu.Haishauriwi kwenda kutembelea eneo hilo
kama hauna uhusiano na watukama Alcides Mendes, mwanzilishi na Raisi wa
Espaco Jovem, taasisi ya vijana ambayo ilimsaidia Nani kuwa mbali na
uhalifu baada ya kutenganishwa na wazazi wake ambao alitoka nao katika
Visiwa vya Carpe Verde vilivyopo barani Afrika akiwa na umri mdogo
kabisa.
Baba
yake Domingos alirudi Santa Filomena on holiday wakati Nani ana miaka 7
na tangu wakati huo hakuwahi kurudi.Mama yake Maria do Ceu aliondoka
Ureno na kwenda Uholanzi Nani alipokuwa na miaka 12, na kumuacha Nani
akiishi na Aunty yake Antonia pamoja na familia yake, wakiwa wanalala
watu sita katika chumba kimoja.
Kupitia
madirisha ya nondo unapata nafasi ya kuona vizuri njia ya reli ambayo
Nani angetembea kwa miguu kwa umbali wa maili 6 kwenda mazoezini na
klabu yake ya kwanza Real Massama.Muda mwingine, kama alikuwa
amechelewa, basi alidandia treni na kumkwempa kondakta.On the other
hand, umbali wa mwendo wa dakika 2 kutoka nymbani kwao kulikuwa na
uwanja mdogo wa kuweza kuhimili wachezaji watano uwanjani - uwanja ambao
alijifunza soka la mtaani.
“Hilo soko kubwa kwetu,” anasema Pereira. “Watoto wa kiafrika kama Nani.Hata unaweza kuona anavyochanganya high level performance na tricks kutoka mtaani.”
Hapa
ndipo Nani alipojifunzia namna ya kutumia miguu miwili, ubora
anaoutumia kuonyesha kipaji chake katika wing ya kulia @ Manchester
United.
“Nilikuwa
natumia masaa kulenga sehemu ya duara kwa kutumia miguu yangu
miwili,nilikuwa nataka sana kujua kucheza vizuri kwa kutumia miguu yangu
yote,” anasema Nani.
Kati
ya takribani watoto maskini 80 in Santa Filomena, Alcides Mendes
anakumbuka Nani ndiye alikuwa mtoto pekee ambaye hakuacha kuzimbikiza
ndoto zake.
“Nani
alikuwa na mtindo wa kuchagua wachezaji dhaifu kwa upande wa timu yake
ili muda wote aweze kumiliki mpira yeye,’ anasema Mendes. “Kwenye pitch
walikuwa wanacheza wachezaji watano watano(mtoano), na mshindi anabaki
uwanjani kucheza na watano wengine, na muda mwingine timu yake
ilipofungwa alikuwa anakasirika sana. Akili yake ilikuwa katika kushinda
tu. Muda wote alikuwa anataka kushinda na kuendelea kucheza tu, nothing
else.
“Ilikuwa
ni vigumu sana kwa watoto kujua ulimwengu nje hapa. Tatizo ni kwamba
hapa watu wengi waishio hapa sio wahamiaji lakini pia sio Wareno pia.
“Wamezaliwa
hapa lakini wazazi wao wanatokea katika makoloni ya zamani ya Ureno
kama Cape Verde, hivyo wanakuwa wanatengwa na jamii (Nani hakupata uraia
wa Ureno mpaka alipofikisha miaka 18).Hata mashuleni kuna madarasa
maalum kwa ajili yao.
“Nyumba
aliyokuwa anaishi Nani ilikuwa ndogo lakinifamilia yao ilikuwa ina
umoja sana na walikuwa na mahusiano mazuri katika yao. Kaka yake mkubwa
alikuwa mtu muhimu sana kwake. Alikuwa anafanya kazi katika ujenzi na
muda mwingine Nani alikuwa naenda kumsaidia kazi.”
Pamoja
na ugumu wa maisha, Nani ana kumbukumbu nzuri kuhusu makuzi yake.
Mchezo mwingine aliokuwa anaupenda akiwa na taasisi ya Espaco Jovem,
ulikuwa ni Capoeira, muunganiko wa Brazilian martial art na music.Hata
tabia yake ya kuruka someraults (sarakasi) ambayo ndio huifanya kila
anapofunga ni kitu ambacho ni cha kawaida sana katika mitaa ya Santa
Filomena.
“Rafiki
zangu walisema nilikuwa kichaa lakini nilikuwa nataka kupata kitu
Fulani kutoka capoeira na ndio maana siku zote nashangilia kwa kuruka
sarakasi,” alisema Nani katika mahojiano ya TV in Portugal wiki nne
zilizopita. “Watu siku zote walikuwa wanazungumza kuhusu Nani(jina
alilopewa na dada zake), yule mtoto mwenye nywele za curly.
“Maisha
yalikuwa magumu lakini ya furaha. Tatizo pekee lilikuwa njaa. Tulikuwa
na hali mbaya sana nyumbani, hukukuwa na chakula, alikuwa kaka yangu
Paulo ambaye alileta chakula kidogo nyumbani.
“Tulifikia
hatua ya kuiba matunda na vitu vingine vya kula. Nilienda katika tabia
zisizo nzuri lakini siku zote nilifanikiwa kurudi katika mstari
ulionyooka.
“Hauwezi
kubadilisha wala kuuficha ukweli huu ya maisha yako ya zamani, na sioni
aibu juu ya sehemu nilipozaliwa au maisha magumu niliyopitia. Kama
nimefika hapa nilipo ilikuwa kwa sababu ya juhudi zangu na moyo wangu wa
kujituma.”
Nani
anakataa kwamba baba yake alimtekeleza, anasisitiza sheria na kanuni za
Ureno zilizomzuia kurudi kwa familia yake.Wanaume hawa wawili
walikutana tena mwaka 2006 na Nani anakumbuka: “Alijaribu kunielezea
kwamba hakunitekeleza, lakini nilimzuia asiendelee na mazungumzo yale na
nilimwambia: “Hauhitaji kujieleza, nipo poa.Nina furaha, nafahamu kilichotokea, hivyo hahitaji kunielezea chochote.”
“Sikuwa
namkumbuka sasa kwa sababu kaka Zangu alikuwa katika nafasi yake.
Walinipa kila aina ya sapoti na mapenzi. Nilikuwa mdogo, nalindwa na
hakuna aliweza kunigusa.”
Nani
hajasahau kipindi alipokuwa anategemea timu yake yake ya Real Massama
kwa ajili ya chakula na rafiki zake kwa ajili ya nguo.
“Nilikuwa
na marafiki wengi waliokuwa wananisaidia sana na kunisapoti kwa sababu
nilikuwa na maisha magumu. Nilikuwa sina uwezo wa kununua nguo nzuri
hivyo rafiki zangu walinipa zile ambazo walikuwa hawazivai tena.
Sometimes walikuwa wananialika kwenda kukaa kwao hata wiki.
“Nilikuwa mtoto wa Real Massama.Walinipa kila kitu-viatu na chakula.Nilikuwa Napata huduma kuliko mtu yeyote katika klabu ile.”
“Ni
kweli alifanya mazoezi na Benfica na Sporting,” anasema Dias. “Benfica
waliwapeleka Massama kucheza katika uwanja mkubwa mbele ya mashabiki
wote kabla ya mchezo wao na Boavista.
“Lakini
mvua ilikuwa inanyesha sana siku hiyo na Souness alisema watoto
hawatocheza kwa sababu wangeharibu majani.Unapotoa ahadi kwa mchezaji wa
umri wa namna ile, unatakiwa kuitimiza, lakini Benfica walishindwa.
“Baada
ya muda kidogo, walimfuata Nani kwa ajili ya kumsajili lakini Nani
alifikiri hawakuwa na heshima kwake .Hakutaka kuwa bidhaa kwa Benfica.
Ingawa alikuwa maskini lakini Nani na kiburi sana.”
Katika
kutambua machungu ya Nani ya kubeba viatu vyake katika mfuko wa
plastiki (Rambo), Dias aliandaa mchango kutoka kwa wachezaji wakubwa
kumchangia Nani pesa ananunue mfuko mzuri.Ilikuwa ni moja ya sehemu ya
special attention aliyokuwa akipewa Nani.
“Nilikuwa
zaidi ya kocha, nilikuwa saikologisti, daktari, na dereva sometimes.
Nilijua kazi yangu haikuwa kumfundisha tu. Pia nilitakiwa kuwa mwalimu
wake, ku-control chakula anachokula, wapi alikuwa analala, kwenda shule
na kuhakikisha alikuwa anaudhuria darasani. Hivi ni vitu ambavyo wazazi
wanafanya.
“@
Massama, alikuwa anakula chakula cha mchana kabla ya mazoezi na kula
dinner baada ya hapo. Kilikuwa ni kitu ambacho watoto wengine hawapati.
Kama alikuwa hajakula akiwa klabuni basi asingekuwa amekula kabisa.”
Ni
mwendo wa nusu saa kutoka Lisbon, kusini maili 11 kutoka katika daraja
la Vasco da Gama na mdomo wa mto Tagus, kabla hujafika vijijini around
Alcochete, ndipo mahali Nani alipong’arisha kipaji chake.
Hapa ndio kilipo chuo cha Academica do Sporting Clube de Portugal.
Ni
takribani miaka 10 tangu Sporting walipojenga hii complex, ikiwa na
viwanja saba vilivyokamilika na hotel ya watoto 50 kati ya 130 ambao
wanajifunza mahala pale. Inagharimu zaidi ya £4m kuiendesha academy
hiyo, lakini Diogo Matos, mkurugenzi wa academy, anakisia academy hiyo
tayari imeshaipa klabu ya Sporting faida ya £150 million kupitia mauzo
ya mastaa kama Cristiano Ronaldo na Nani.
“Tuna kitu Fulani maalum kinachoendelea hapa,”
anasema Matos ambaye matunda yake ya sasa ya wachezaji under 19
wameibuka kuwa moja ya timu bora barani ulaya katika michuano ya NextGen
Series(champions league for under19).
Ingawa
iliamuliwa kumbakisha Nani at Massama kwa sababu ya hali ya nyumbani
kwao, lakini alikuwa akifanya mazoezi na Sporting kabla ya kujiunga na
klabu hiyo akiwa na miaka 16. Nani alivuna mshahara wa £900 kwa mwezi
akiwa kama mchezaji wa academy, lakini aliibuka kupata £10,000
aliposaini kama professional.
Pesa
hiyo ilitumika kumuhamisha aunt yake Antonia nje ya Santa Filomena, na
ameendelea kuisapoti familia yake kiuchumi hadi sasa anapopata mshahara
mkubwa akiwa na United.Ni mzigo ambao Nani anapenda kuubeba lakini
anakiri, hali hii imekuwa ikiingilana na career in premier league.
“Namshukuru
Mungu kwa hali yangu ya sasa na mimi ni nguzo katika familia yangu.Kila
linapotokea tatizo wanakuja kwangu mimi na sijawahi kusema
hapana.Nafahamu wapi nilipitia kipindi nilipokuwa mdogo.Sipendi kuona
mtu yeyote katika familia yetu akiwa na shida.
“Lakini
matatizo binafsi yananifanya nipoteze umakini. Muda mwingine kiakili
nachoka kabisa. Inaweza kuwa hata kabla ya mechi kubwa au derby, lakini
nitapokea simu na kumpigia yeyote anayehusika kutatua tatizo lolote
linaloikumba familia yangu.
“Napata pesa nyingi lakini hazikushuka tu kutoka mbinguni. Lazima nijitume. Nisipocheza vizuri, watu watanifukuza.”
Maisha
nchini England hayakuwa mapesi kwa Nani. Ilichukua muda kupata imani
kutoka kwa mashabiki na kuibuka kutoka kwenye kivuli cha Ronaldo at
United. Kulikuwa na kipindi ambapo wasiwasi wa Queiroz juu ya Nani
kuweza kumudu kucheza Old Trafford ilianza kuchukua nafasi.
Hata
baada ya kuongoza kwa kutoa asisists nyingi msimu uliopita, alijikuta
akiwa kwenye benchi katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa wa
ulaya dhidi ya Barcelona, na kuwasili kwa winga wa kiingereza Ashley
Young kipindi cha kiangazi kulizusha speculations kwamba mreno huyo
angeweza kuondoka Old Trafford.
In
fact, Nani amethibitisha ubora wake akiwa na United msimu huu. Ana
furaha nje ya uwanja na hata nyumbani kwake – Cheshire ambapo anakaa na
mpenzi wake Daniela na mbwa wao wawili.
“Sikuwa
na bahati nzuri kuzoea maisha ya England, tena ilikuwa vigumu sana
kuishi peke yangu, huku nikiwa sijui kuongea lugha ya pale. Ilifikia
kipindi nilikuwa naishi kwa Cristiano na nilijisikia vizuri sana
Kulikuwa kuna watu poa sana na tulikuwa na kila kitu – swimming pool,
Jacuzzi, tennis, kiukweli kipindi nakaa kwa Ronaldo sikuwahi kui-miss
familia yangu.
“Lakini
baadae ilibidi niondoke kwa Ronaldo kwa sababu ilibidi niwe na maisha
yangu. Ilikuwa vigumu sana kwa sababu ilikuwa nyumba kubwa na usiku
ilikuwa kama nyumba ya mchawi.
“Nilikuwa
naogopa hata kuwa nyumbani. Sometimes sikuwa natoka hata chumbani.
Nilienda kulala mapema bila kula vizuri kwa sababu sikutaka kula dinner
peke yangu.”
Hata
sasa, Nani anakiri, hawezi kuangalia movie za kutisha kwa sababu
zilikuwa zinamfanya asilale kwa woga. Anapenda kukaa na Daniela na
kuangalia tamthilia na kupig piano.
October
2011. Katika uwanja wa Porto Estadio Do Dragao. Nani alifunga mabao
mawili ya mwanzo katika ushindi wa Ureno wa 5-1 dhidi ya Iceland, na
kumfunika mchezaji mwenzie Ronaldo. Siku iliyofuata katika kurasa za
mbele za gazeti la Correio da Manha na A Bola walieka picha zake akiwa
anashangilia.
Mtoto kutoka Santa Filomena ametoka mbali sana.
No comments:
Post a Comment