UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA WATISHIA MAISHA YA WANAFUNZI WAISHIO HOSTEL ZA NJE SAUT MWANZA
Matukio ya unyang’anyi yamekuwa yakitokea maeneo ya Chuo cha Mtakatifu A
gustino ambapo baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakinyang’anywa vitu vyao vya thamani na hata kujeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali.
Siku ya Jumatatu tarehe
24/10/2011 majira ya saa nne za usiku mabinti watatu walivamiwa maeneo
ya karibu na hosteli za chuo hicho za Rugambwa, ambapo kati yao wawili
waliojulikana kwa jina moja moja ni Getrude na Neema,wanafunzi wa
shahada ya masomo ya jamii mwaka wa 3 (BA. in Sociology) na tukio
lingine ni la mwanafunzi wa shahada ya mawasiliano ya umma mwaka wa 3
(BA. in Mass Communication) Jaysam Jeremiah lililotokea tarehe
25/10/2011 majira ya saa 5:30 usiku siku moja baada ya kutokea tukio la
kwanza ,Jaysam alijeruhiwa mkononi na kutibiwa zahanati ya chuo usiku
huo huo.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo
Jaysam amemuomba mkuu wa jeshi la polisi Mkoani Mwanza Kamanda Libelatus
Baro kwa kushirikiana na Uongozi wa Chuo cha Mtakatifu Agustino
kuimarisha Ulinzi maeneo ya Malimbe ambapo idadi kubwa ya wanaoishi
maeneo hayo ni Wanafunzi wa chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino, “unajua
ulinzi chuoni hapa upo ndani ya chuo kutokana na chuo kuajiri kampuni ya
ulinzi ndani ya chuo, lakini sisi wanafunzi tunaoishi nje ambao ni
wengi tumekuwa hatuna ulinzi kabisa na hivyo hujikuta tukivamiwa na
wahalifu katika hosteli zetu na hata usiku wakati tunatoka chuoni
kujisomea”, alisema Jaysam.
Katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu
Agustino, Mwanza karibia robo tatu ya wanafunzi wa chuo hicho zaidi ya
10,000 wanaishi katika hostel za nje ambazo zipo maeneo ya jirani na
chuo hicho kutokana na uhaba wa hostel za ndani zinazomilikiwa na chuo
hicho. Matukio kama hayo yamekuwa yakiripotiwa kutokea hasa kwa
wanafunzi wanaoishi hosteli za nje ya chuo kutokana na ulinzi wa maeneo
hayo kutokuwepo hivyo kutoa mwanya kwa wahalifu kufanya uhalifu kwa
wanafunzi hao.
No comments:
Post a Comment