Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
ameiambia BBC kitengo cha michezo, klabu hiyo imeanza mazungumzo na
Robin van Persie kuhusiana na mkataba mpya.
Robin van Persie
Alipoulizwa moja kwa moja iwapo anafanya mazungumzo na Van Persie, Wenger alijibu: "Ndio".
"Amebakisha miezi 18 kabla ya mkataba wake wa sasa kufikia ukingoni na ninahakika atasaini mkataba mpya."
Van Persie ndiye mchezaji pekee wa Arsenal aliyebakia katika kikosi hicho ambaye aliyewahi kushinda kikombe akiichezea timu hiyo.
Meneja wa Arsenal anatarajiwa kufanya kila awezalo kumbakisha mpachika mabao wao huyo hodari baada ya kuondoka msimu huu wachezaji muhimu Samir Nasri, Cesc Fabregas na Gael Clichy.
Hata hivyo, Wenger alifanikiwa kuwachukuwa wachezaji wawili wa kiungo Yossi Benayoun na Mikel Arteta, wakati mlinzi Per Mertesacker na mshambuliaji Ju-Young Park pia waliongezwa katika kikosi cha timu hiyo.
No comments:
Post a Comment