BOBAN AITWA KWENYE KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS
28 WAITWA KILIMANJARO STARSK
kocha
Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface
Mkwasa ameteua wachezaji 28 kuunda kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya
Kombe la Chalenji inatakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Novemba 25
mwaka huu. Wachezaji walioteuliwa ni Juma Kaseja (Simba), Deo Munishi
(Mtibwa Sugar) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni Shomari
Kapombe (Simba), Godfrey Taita (Yanga), Juma Jabu (Simba) na Paul
Ngelema (Ruvu Shooting). Mabeki wa kati ni Juma Nyoso (Simba), Said
Murad (Azam), Erasto Nyoni (Azam) na Salum Telela (Moro United). Viungo
ni Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Ibrahim Mwaipopo (Azam), Nurdin Bakari
(Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba), Haruna Moshi (Simba), Ramadhan Chombo
(Azam), Rashid Yusuf (Coastal Union), Jimmy Shogi (JKT Ruvu Stars) na
Mohamed Soud (Toto Africans). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Azam),
Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC),
Gaudence Mwaikimba (Moro United), John Bocco (Azam), Thomas Ulimwengu
(TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Hussein Javu (Mtibwa
Sugar), Daniel Reuben (Coastal Union) na Nizar Khalfan (Vancouver
Whitecaps, Canada).
MAPATO STARS v CHAD
Pambano
la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014
nchini Brazil- raundi ya mtoano kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Chad
lililochezwa Novemba 15 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
limeingiza sh. 78,389,000. Mashabiki waliokata tiketi kushuhudia pambano
hilo ni 29,111. Viti vya kijani na bluu ambavyo kiingilio kilikuwa sh.
2,000 ndivyo vilivyovutia mashabiki wengi ambapo walikuwa 23,748 ikiwa
ni zaidi ya asilimia 80 ya mashabiki wote walinunua tiketi kwa ajili ya
viti hivyo. VIP A ambapo ndipo kulikokuwa na kiingilio cha juu cha sh.
20,000, jumla ya mashabiki 187 walinunua tiketi kwa ajili ya eneo hilo.
VIP B ambapo kiingilio kilikuwa sh. 10,000, mashabiki walionunua tiketi
walikuwa 1,181. Viingilio vingine katika pambano hilo vilikuwa sh. 5,000
kwa VIP C ambapo waliingia mashabiki 1,678 wakati mashabiki 2,319
walikata tiketi kwa viti vya rangi ya chungwa ambapo kiingilio kilikuwa
sh. 3,000.
VIONGOZI WALIOCHAGULIWA KUONGOZA FAM
Uchaguzi
wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM) ulifanyika
Novemba 13 mwaka huu wilayani Rorya. Uchaguzi huo uliendeshwa na Kamati
ya Uchaguzi ya FAM chini ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF). Viongozi waliochaguliwa kwa kuzingatia Katiba ya
FAM na Kanuni za Uchagzui za wanachama wa TFF ni wafuatao; Fabian Samo
amefanikiwa kutetea wadhifa wake wa Mwenyekiti huku Deogratius
Rwechungura akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti. Wengine waliochaguliwa
ni Mugisha Galibona (Katibu Mkuu), Samwel Silasi (Katibu Msaidizi),
Evans Liganga (Mhazini), David Sungura (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF),
William Chibura (Mwakilishi wa Klabu) na Valerian Goroba (Mjumbe).
No comments:
Post a Comment