DAH! kweli MTV noumaaaaaaaa!!!
huyu
ndio jamaa aliyejitokeza akiwa UCHI, mbele ya maelfu ya watu
waliohudhuria na mamilioni ya watu waliokua wanatazama LIVE kwenye TV.
yako matukio mengi, lakini moja la mwaka jana ni wakati mcheza mieleka mmoja alipopanda kutoa tuzo ambapo kabla ya kuitoa, alisema watu wote wanaomkubali na kumpenda shetani wanyanyue mkono juu na kuweka alama ya mapembe kwa kutumia vidole kama kumtukuza na kumsalute Mungu wao yani shetani.
kweli watu walinyanyua mikono na kuweka alama hiyo ya mapembe ambayo inatumika kama moja ya alama za watu wanaoabudu kwenye dini ya usiku, dini ya kishetani.
sasa mwaka huu, moja kati ya vituko vilivyotokea ni wakati tuzo ya wimbo bora wa mwaka ilipokua ikitolewa kwenye tuzo hizo za MTV EUROPE jana usiku, ambapo alijitokeza mshkaji ambae sikuweza kumshika jina mara moja, lakini alijitokeza uchi kabisa, kitendo kilichofanya madem kupiga kelele na ukumbi mzima kumgeukia yeye, huku mamilioni ya watazamaji wakichek LIVE kupitia MTV.
kwa nini naamini hichi kitu kilipangwa? ni kwamba huyu mshkaji alitokea backstage wanapokaa wasanii wote na wengine wanaohusika kupanda kwenye stage kwa wakati huo, kula kuna walinzi na wasimamizi zaidi ya 10, ina maana hawakumuona? kwa sababu alipita watu wengi pia mpaka kufika kwenye stage.
show ilikua inarushwa LIVE kwenye TV, naamini kama kilikua ni kitu ambacho MTV hawakukitarajia, ni lazima wangefanya juu chini huyu jamaa aondolewe hata kwa mabaunsa kumfata kati kati ya stage, kwa sababu alikaa kama dakika tatu mpaka nne kwenye hiyo stage.
No comments:
Post a Comment