Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, November 29, 2011

JOH MAKINI ajibu kauli ya B HITS!


Joh Makini
Mfalme kutoka kaskazini, staa wa single ya bye bye rappa Joh Makini amezungumza exclusive kwenye amplifaya jana baada ya kauli iliyotolewa na uongozi wa studio ya B HITS iliyohusika kuitengeneza hiyo single ya bye bye.
boss wa b hits music group Hermy B, aliandika jana kwenye facebook kwamba “Joh Makini umeikasirisha B’Hits, Wimbo wa bye bye tulikupa bure baada ya kutujibu kwa dhihaka tulipodai malipo yetu, Hata kutupa Credit zetu kwenye video umeona kazi pia, ama kweli shukrani ya punda ni mateke, we mtu gani? Kumbuka ulipotoka!!!
Hizo ni lawama kwamba, audio ya bye bye ilitengenezwa na b hits lakini kwenye video iliyotengenezwa na Adam wa Visual Lab, B hits haikuandikwa kama ndio imehusika kuitengeneza.
Joe Makini akizungumza na AMPLIFAYA ya Millard Ayo, amesema “sidhani kama kuna matatizo yoyote kati yangu na B HITS kwa sababu hata jana nilikua na Producer wao PANCHO LATINO, na kilichotokea ni bahati mbaya tu Adam hakuandika B HITS kwamba ndio wamehusika kuitengeneza hiyo AUDIO, hata hivyo sisi wenyewe hatukutegemea kama ingekua kitu kikubwa hivi na kuleta mvutano mkubwa kama huu, ni kitu ambacho ni cha kurekebishwa tu kirahisi” – JOH MAKINI
amemalizia kwa kusema nimeanza kusambaza video ya bye bye ambayo tayari Adam ameshaifanyia marekebisho na kuiandikia jina la B HITS, kuanzia leo na kesho ndio hiyo kazi ya kuzisambaza inafanyika.
Hermy B
KWA HISANI YA MILLARD AYO

No comments:

Post a Comment