
Wakati kikosi cha Taifa Stars,
kikiingia kambini jana kujiandaa na mechi ya mchujo dhidi ya Chad
itakayochezwa Novemba 11 jijini N’Djamena, kocha wa timu hiyo, Jan
Poulsen, amemtema mshambuliaji Dan Mrwanda na kumuita John Bocco
‘Adebayor’ wa Azam FC kuziba nafasi yake.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Poulsen alisema amemua kumuacha mchezaji
huyo anayekipiga katika klabu ya DT Long An, Vietnam kutokana na
kutokuwa na uhakika kama atajiunga na wenzake kwa wakati kwani muda wa
kujiandaa kabla ya mechi hiyo ni mdogo.
Stars inatarajiwa kuondoka
nchini kwenda Chad Novemba 9 kwa ajili ya mchezo huo kabla ya kurudiana
Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam kuwania kuingia kwenye makundi
ya kusaka tiketi ya fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014.
Kikosi
hicho kinaundwa na Makipa, Juma Kaseja (Simba), Mwandini Ally (Azam
Fc). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam Fc), Juma Jabu na Juma Nyoso (Simba),
Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya), Erasto Nyoni (Azam Fc), Nadir Haroub
‘Cannavaro’ na Godfrey Taita (Yanga).
Viungo
ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga),
Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam),
Ramadhan Chombo (Azam Fc) na Shomari Kapombe (Simba).
Washambuliaji ni, Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps,
Canada), Mrisho Ngassa (Azam Fc), Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata (TP
Mazembe, DR Congo), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) na Hussein
Javu (Mtibwa Sugar).
No comments:
Post a Comment