Kiongozi wa tawi la vijana la
chama cha ANC, Afrika Kusini, Julius Malema -- anahudhuria kikao cha
mwisho leo kutazama vitendo vyake.
Kisa hicho kilianza pale Bwana Malema alipotoa wito kuwa serikali ibadilishwe katika nchi ya jirani ya Botswana.
Ameomba msamaha kwa matamshi hayo.
Julius Malema alikuwa akimuunga mkono Rais Zuma tangu alipochukua uongozi wa chama, lakini wanasiasa hao wawili sasa hawapatani.
Matokeo ya vikao hivyo vya chama yatatolewa baada ya siku kadha.
No comments:
Post a Comment