Pages

Friday, November 25, 2011

NIZAR KHALFAN AJIUNGA NA PHILADELPHIA UNION.

Klabu ya Vancouver Whitecaps ya nchini Canada inayoshiriki Ligi kuu nchini Marekani imemtoa kiungo wa kimataifa toka Tanzania Nizar Khalfan kwenda kwenye klabu ya Philadelphia Union ambayo kama Whitecaps inashiriki ligi ya MLS . Whitecaps imemruhusu Nizar kwenda Philadelphia katika mchakato wa maalum wa kubadilishana wachezaji wa ligi hiyo maarafu kama Waver Player Draft.
Nizar Khalfan ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Mtwara, ameichezea Whitecaps katika michezo 22 ya ligi ya MLS kwa mwaka 2011 ambapo alianza michezo 9. Katika dakika 1,066, kiungo huyu mwenye umri wa miaka 23 alifunga bao moja huku akitoa pasi 4 za mabao kwa wenzake .


Nizar alijiunga na Whitecaps katikati ya msimu wa mwaka 2009 wakati klabi hiyo bado ikiwa kwenye ligi daraja la kwanza na kwa jumla amecheza michezo 58 ambayo ni sawa na dakika 3,029 .
Khalfan alianza soka lake nchini Tanzania akiwa na klabu ya Mtibwa Sugar kwenye msimu wa mwaka 2005/06 na katika msimu wa mwaka 2006-7 aliichezea Moro United.


Katika misimu hiyo miwili Nizar alicheza michezo 57 akifunga mabao 16 akiwa na Mtibwa na mabao matano katika katika michezo 16 akiwa na Moro United. Katikati ya misimu hiyo miwili Nizar alicheza soka la kulipwa nchini Kuwait
Khalfan ameichezea timu ya taifa ya tanzania Taifa Stars katika michezo 25 ya kimataifa na amefunga mabao matano,

Khalfan alifunga bao la ushindi katika mchezo wa kihistoria dhidi ya Burkina Faso kwenye uwanja wa taifa wa Dar es salaam tarehe 2 septemba 2006 kwenye uwanja wa taifa Dar es salam, na pia alifunga bao la nne kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya Mauritius septemba 6 mwaka 2008.
Hivi karibuni Khalfan aliichezea timu yake ya taifa katika mchezo wa kufuzu kwa mataifa ya afrika ambapo alitoa pasi ya bao lililofungwa na Mbwana Samatta kwenye mchezo dhidi ya Algeria ulioisha kwa sare ya 1-1, na pia alianza kwenye michezo yote miwili ya awali ya kufuzu kwa kombe la dunia 2014 ambako timu yake ilifuzu kuingia kwenye kundi lenye timu za Ivory Coast, Morocco na Gambia.

No comments:

Post a Comment