POLISI ARUSHA WAMSHIKILIA DKT SLAA,TUNDU LISU, MBOWE NAYE ASAKWA NA POLISI
NA GLADNESS MUSHI, ARUSHA
Jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia wafuasi wa chadema 20 akiwemo katibu wa chama cha chadema Dkt Wilboard Slaa pamoja na mbunge wa Singida Bw Tundu Lissu,huku mwenyekiti wa chama hicho Bw Freeman Mbowe akiwa ametoroka na kwa
kosa la kukiuka masharti ya jeshi la polisi cha kufanya mkutano wa
hadhara kwa masaa matano na badala yake wakakesha katika viwanja vya NMC
mjini hapa kwa ajili ya shinikizo dhidi ya mbunge wa arusha mjini
kinyume cha sheria
Akiongea na vyombo vya habari kaimu kamanda wa jeshi hilo kwa mkoa wa Arusha Bw Akili Mpwapwa alieza kuwa watu hao ambao ni watuhumiwa wanakabiliwa na shitaka hilo kwa kuwa wamekiuka kwa makusudi masharti ya kibali chao
Kamanda
mpwapwa ameendelea kwa kusema kuwa mnamo tarehe saba chama cha
demokrasia na maendeleo kilipewa kibali maalumu cha kuweza kufanya
mkutano wa hadhara katika viwanja vya NMC lakini badala yake chama hicho
kwa kuongozwa na viongozi wa ngazi za kitaifa walipuuzia suala hilo na
kufanya mkesha huku wakiwa wanaendelea kutoa lugha za kejeli kwa
serikali.
Aliendelea
kudai kuwa viongozi hao kwa kushirikiana na wananchi waliamua kufanya
mkesha maalumu juu ya kushinikizwan kuwekwa rumande kwa mbunge wa jimbo la arusha mjini ambapo wafuasi hao walikesha huku kibali cha mkutano huo kikiwa tayari kimeshakiwisha
“Hawa
chadema walivunja utaratibu huo tena kwa kujua kabisa kitu ambacho
kilikuwa kinaendelea kwa kuwa kibali kilikuwa kinajieleza wazi juu ya
kutokusanyika baada ya masaa matano kuisha, kutokashifu dini au chama
kingine,pia kutokuwa na maandamano ya magari au pikipiki lakini
walikiuka agizo hilo alisema Akili.
Kamanda
huyo aliongeza kuwa mara baada ya watu hao kukaa kwa zaidi ya masaa
mengi huku mji ukiwa na tafrani kubwa sana ya kutokea kwa vita polisi
waliamua kuchukua maamuzi kwa maslahi ya wananchi wa Mkoa wa arusha na
hivyo kuweza kuwatanya watu hao.
Pia alisema kuwa viongozi hao wa chadema waliendelea na lugha za kejeli na
kuonesha ukaidi dhidi ya sheria za nchi wakati nao polisi wakiendelea
kuwasihi wasitishe mkuatano huo ambao ulidumu mpaka alfajiri lakini bado
viongozi hao walikiuka amri hiyo.
Aliongeza
kuwa mnamo majira ya alfarjiri polisi walilazimika kutumia mabomu ya
machozi ili kuweza kuwatanya watu jambo ambalo nalo lilifanikiwa kwa
kiwango cha hali ya juu sana na wafuasi hao wakaweza kukimbia na
kutawanyika katika eneo hilo la NMC.
‘tulipoingia
uwanjani hapo na kutumia zaidi nguvu watu walikimbia sana lakini bado
sisi tulilenga kuwakamata baadhi ya watu wakiwemo viongozi
wa chama hicho ambapo Dkt slaa alikutwa akiwa amejificha chini huku
Mbunge wa singida Tundu Lisu naye akijisalimisha kwa jeshi la polisi,
mwenyekiti wa chama hicho akitokomea kusikojulikana”aliongeza kamanda
Mpwapwa.
No comments:
Post a Comment