Pages

Wednesday, November 9, 2011

UJIO WA PRINCE CHARLES ZANZIBAR KATIKA PICHA

UJIO WA PRINCE CHARLES ZANZIBAR KATIKA PICHA

Mtoto wa Malkia Elizabeth 11 Prince Charles akiwa na mkewe Duchess of Conrnwall wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa ziara ya kutwa moja PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBARI.
Rais wa Zanzibar akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakitowa zawadi kwa Mtoto wa Malkia Elizabath 11 Prince charless pamoja na mkewe Duchess of Conrnwall hapo Ikulu Mjini Zanzibar.
Prince Charles akiwa na mkewe Duchess of Conrnwall waliovaa mashada ya mauwa wakipokelewa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd mwenye suti nyeusi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa ziara ya kutwa moja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Moh’d Shein Mwenye suti nyeusi akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake Prince Charles Ikulu Mjini Zanzibar.
Mke wa Prince Charles akiwa ameshikilia Mkoba wa Ukili ambao umetengenezwa na wajasiriamali wa Zanzibar baada ya kuwatembelea na kuangalia kazi zao,wa Mwanzo kulia ni Waziri wa Biashara Viwanada na Masoko Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui.
Prince Charles akisakata ngoma ya Uringe pamoja na Waziri wa Biashara Viwanada na Masoko Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui mwenye suti nyeusi katika Viwanja vya Ngome Kongwe Mjini Zanzibar.
Prince Charles na Mkewe wakikabidhi msaada wa Vyandarua kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk. Saleh Ahmed Jidawi mwenye Shati Jeupe.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Moh’d Shein akibadilishana mawazo na wageni wake Prince Charles akiwa na mkewe Duchess of Conrnwall, kushotoni kwake ni Mke wa Rais Shein Mama Mwanamwema Shein hapo Ofsini kwake Ikulu Mjini Zanzibar

No comments:

Post a Comment