Pages

Wednesday, December 14, 2011

Anelka ajiunga na Shanghai Shenua


Mshambuliaji Nicolas Anelka atajiunga rasmi na klabu ya Shanghai Shenua mwezi wa Januari kwa mkataba wa miaka miwili baada ya klabu hiyo ya China kukubaliana na Chelsea.
Anelka akiwa na mkurugenzi wa Shanghai Shenua
Anelka akiwa na mkurugenzi wa Shanghai Shenua

Anelka mwenye umri wa miaka 32 alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na aliyekuwa meneja wa Chelsea, Avram Grant mwezi wa Januari mwaka 2008 na aliweza kupachika mabao 59 katika mechi 185 alizochezea klabu hiyo.
Mkataba wake na Chelsea unamalizika mwishoni mwa msimu huu na maombi yake ya uhamisho yalikubaliwa wiki iliyopita.
Shenua tayari imeshaweka picha ya Anelka katika ukurasa wa mbele wa mtandao wake.
Anelka, aliyejiunga na Chelsea kwa kitita cha paundi milioni 15 akitokea Bolton, amekuwa akifanya mazoezi tofauti na wachezaji wa kikosi cha kwanza tangu meneja Andre Villas-Boas alipoafiki maombi yake ya uhamisho.
Msimu huu Anelka amefunga mabao 15 tu, huku Didier Drogba, Daniel Sturridge na Fernando Torres wakichezeshwa zaidi nafasi ya ushambuliaji.
Klabu ya Shanghai Shenua, ambayo ilishuka daraja misimu miwili iliyopita kutokana na kupanga matokeo, lakini ilimaliza nafasi ya 11 kati ya nafasi 16 ya msimamo wa Ligi Kuu ya China msimu uliopita.
Lengo lao ni kushinda ligi na tayari wamesajili washambuliaji kutoka Brazil Cleo na Muriqui, pia wamehusishwa kumchukua meneja Jean Tigana na wanawinda wachezaji wengine maarufu akiwemo Didier Drogba.

No comments:

Post a Comment