Pages

Saturday, December 10, 2011

HAFLA YA KUSHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA YAFANA VIWANJA VYA IKULU USIKU HUU


Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha UDP Bw. John Momose Cheyo katika hafla ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania iliyofanyika usiku huu kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, huku mtandao wako wa FULLSHNAGWE ukikuletea matukio haya kutoka viwanja vya Ikulu moja kwa moja.
Wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali, Mawaziri, Wabunge na Mabalozi na waalikwa mbalimbali wamehudhuria katika hafla hiyo iliyokua na burudani za vikundi vya ngoma kutoka sehemu mbalimbali.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na wageni waalikwa wakati alipokuwa akipita sehemu mbalimbali na kuwasalimia katika viwanja vya Ikulu huku akiwatakia sherehe njema ya miaka 50 ya Uhuru.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion na magazeti ya Dira na Hekaheka Viwanjani Bw. Alex Msama ambaye naye alihudhuria katika hafla hiyo.
Waimbaji wa muziki wa injili nao wamehudhuria katika hafla hiyo kama wanavyoonekana katika picha.
Kikundi cha ngoma kiktumbuza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion na magazeti ya Dira na Hekaheka Viwanjani Bw. Alex Msama akibadilishana mawazo na Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dk Emmanuel Nchimbi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion na magazeti ya Dira na Hekaheka Viwanjani Bw. Alex Msama akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu - Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. William Lukuvi katika hafla hiyo.
Wadau wa Double Tree walikuwepo katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na wageni waalikwa katika hafla hiyo iuliyofanyika viwanja vya Ikulu usiku huu
Wakuu wa taasisi mbalimbali za Serikali walikuwepo kutoka kulia ni Clement Mshana Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Helman Hokororo, Mkuu wa vikosi vya Zimamoto ACF Fikiri S. Salla, mdau Esther Baruti na mpiga picha wa Idara ya habari Maelezo John Lukuwi wakijadili jambo.
Mdau John Melele Mkuu wa Utawala CCM makao makuu Ofini ndogo Lumumba akiwa na Nancy Mukoyogo kulia na Upendo Mazzuki nao wamehudhuria katika hafla hiyo ya miaka 50 ya uhuru.
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Alberic Kacou katika viwanja vya ikulu wakati wa hafla ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania iliyofanyika usiku huu jijini Dar es salaam.
Wadau kutoka vyombo mbalimbali nao walihudhuria mnuso huo katika viwanja vya Ikulu.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika viwanja vya ikulu katika hafla ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.
Kundi la muziki wa Taarab likitumbuiza katika viwanja vya ikulu wakati wa hafla ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania iliyofanyika usiku huu jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment