Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, December 10, 2011

UNIC YATOA MAFUNZO KWA VIJANA JUU YA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA KULINDA HAKI ZA BINADAMU.


:Afisa Habari wa UN Information Centre (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akiwakaribisha wageni waalikwa katika semina ya mafunzo kwa vijana juu ya matumizi ya mtandao katika kuhamasisha haki za Binadamu iliyofanyika katika Ofisi za UN Information Centre.
Afisa Habari wa United Nation Information Centre Bi. Stella Vuzo akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kuhusiana na Azimio la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwaka 1948 lenye vipengele 30 ambavyo vimeainisha Haki Msingi za Binadamu na Uhuru.
Mtaalamu wa IT na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu kutoka Kamisheni ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Bw.Wilfred Warioba akielezea jinsi mitandao ya Kisasa ya Mawasiliano kama vile Facebook, Twitter na Blogs zinavyofanyakazi na zinavyoweza kutumika kupashana Habari na Kuelimishana ambapo pia amesema iwapo itatumika vibaya inaweza kuelta madhara makubwa kwa watumiaji. Katikati ni Mzungumzaji Mkuu Mwalikwa kutoka CHRAGG Bw. Ayoub Rioba na Afisa Habari wa United Nation Information Centre Bi. Stella Vuzo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka Shule za Chang'ombe, Ruvu Sekondari, IST, Kibasila, Loyola na TEYODEN wakifuatilia mafunzo hayo.
Mwanafunzi wa Kidato cha Tano Janeth Absalom kutoka Loyola High School akichangia mada wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Habari wa Temeke Youth Development Network (TEYODEN) Humphrey Shao akifafanua jambo kuhusiana na matumiz ya mitandao kama njia ya mawasiliano.
Wanafunzi wakiwa wameshika Poster yenye Ujumbe maalum unaonyesha kwamba Binadamu wote ni sawa bila kujali aina ya Ulemavu mtu alionao.
Mgeni rasmi katika mafunzo hayo Vicky Ntetema kutoka Taasisi inayotetea haki za jamii ya watu wenye Ulemavu wa Ngozi ya Under the Same Sun akieleza jinsi watu wengine wanavyoweza kutumia mitandao hiyo kukiuka haki za msingi za Binadamu kwa namna mbalimbali na kuwataka vijana kuwa makini na kuepuka kupeana ahadi za kukutana na watu wasiowajua waliowasiliana nao kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter na Blogs.

No comments:

Post a Comment