Pages

Friday, January 13, 2012

BEI YA UMEME YAONGEZWA



makao makuu ya TANESCO, Ubungo Dar es salaam.

WAKATI gharama za maisha kwa Watanzania wengi zikizidi kupanda kila siku, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeidhinisha ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 40.29 kwa Tanzania Bara na asilimia 28.21 kwa Zanzibar kuanzia Januari 15, mwaka huu.
Kutokana na kupanda kwa kiwango hicho, watumiaji wa umeme wa majumbani wanaotumia zaidi ya unit 50 kwa mwezi watanunua kila uniti kwa sh 273 badala ya sh 155 na watumiaji wakubwa wa viwandani watanunua uniti moja kwa sh 118 badala ya sh 84.
Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu ndio alitangaza huo mpango kujibu maombi ya dharura ya TANESCO ya kutaka kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 155 ambapo Bodi ya Wakurugenzi ya Ewura imeamua kupandisha gharama za umeme kwa kiwango hicho, ili kuwepo kwa uwiano wa faida kati ya watumaji na TANESCO.
maombi yalikua mengi lakini hawakuyakubali yote kwa asilimia 100 kutokana na baadhi ya sababu walizoziainisha kutokuwa na vielelezo vya kuthibitisha kwamba “Kuna mambo mengi walisema ni ya dharura, lakini baada ya kuyapitia na kuwahusisha wadau mbalimbali tukayapunguza kwa sababu hayakukidhi haja, Mfano walikisia kwamba mwaka huu hautakuwa na mvua kabisa, lakini tulipowasiliana na Mamlaka ya Hali ya Hewa walituambia hilo halina ukweli, hivyo tukaona hatuwezi kuishi kwa hisia tu, – Haruna
amemalizia kwa kusema kwamba gharama zimepanda kwa kiwango hicho baada ya serikali kuamua kufuta kodi ya mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme, ili kusaidia kupunguza ugumu wa maisha ambapo gharama hizo za umeme zitadumu kwa miezi sita na kwamba wakati huo kutakuwa na mtaalamu wa kufanya uchambuzi wa kina kutathmini gharama halisi za umeme zinazopaswa kutozwa nchini.
stori kutoka FREEMEDIA

No comments:

Post a Comment