Pages

Monday, February 6, 2012

KADANSE FC YA WANAMUZIKI YAPIGWA 4-3 NA BONGO MOVIE UWANJA WA TAIFA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik akimkabidhi kombe Nahodha wa timu ya Bongo Movie Vicent Kogosi (Ray), katika mchezo wa wanamuziki na waigizaji uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaa leo, ili kuchangia wahanga wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni jijini Dar es salaam na kusababisha vifo na uharibifu wa mali, mgeni wa heshima katika pambano hilo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik, wengine katika picha kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya kipolisi Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova Bongo Movie yaani waigizaji wameshinda magoli 4 wakati timu ya Kadanse FC ambayo imepata magoli 3 hivyo kufanya mpambano huo kumalizika kwa Bongo Movie kuchukua kombe la mashindano hayo ya kuchangia wahanga wa mafuriko ya Jangwani ambapo mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndiye aliyekabidhi kombe hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akiwa katika picha ya pa,moja na wachezaji wa timu ya Bongo Movie mara baada ya kuishinda Kadanse FC goli 4-3 kwenye uwanja wa Taifa leo.
Wachezaji wa Bongo Movie wakishangilia mara baada ya ushindi huo.
Mmoja wa waigizaji namashabiki wa Bongo Movie akimwaga mauono mbele ya mashabiki waliojitokeza katika mchezo huo uwanja wa Taifa.
Refarii wa mchezo wa leo Bw. Othman Kazi akikabidhi kombe kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Said Meck Sadik ili naye akabidhi kwa washindi wa mchezo huo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik akiingia kwenye uwanja wa Taifa tayari kwa kutoa kombe kwa washindi mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kulia ni Kamanda wa Kamda maalum ya Kipolisi Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova na kulia ni Kamishna Jamal Lwambo.
Rich Mtambalike "Rich Rich" kulia pamoja na Steven Nyerere wakimwaga mauno katika moja ya staili yao ya kushangilia ushindi wa timu yao ya Bongo Movie.
Vimwana wa Bongo Movie wakielekea uwanjani kushuhudia upokeaji wa kombe lao.
Vimwana wa Bongo Movie wakielekea uwanjani ilikuwa burudani kweli.
Wachezaji wa Bongo Movie wakiongozwa na Claudi wakishangilia kuzunguka uwanja mara baada ya mpira kumalizika huku timu yao ikiibuka mshindi kwa kushinda magoli 4-3 dhidi ya Kadanse FC ya wanamuziki.
Mwanamuziki Christian Bella wa bendi ya Akudo Impact katikati akiongozana na wenzake wakatika wachezaji hao waliposawzisha goli lao,
Mwanamuziki wa FM Academia Totoo Kalala akiukokota mpira kiuelekea goli la timu ya waigizaji wakati chezo huo ukiendelea kwenye uwanja wa Taifa.
Hili ndiyo benchi la ufundi la timu ya Bongo Movie likogozwa na Mzee Chilo kushoto, JB Steven, Saimon Mwakifwamba na Cheki Budi.
Benchi la ufundi la Wanamuziki likiongozwa na Asha Baraka wa tatu kutoka kulia waliosimama na kulia ni MCD wa Twanga Pepeta, Yelo Masai wa FM Academia na kushoto ni Jose Mara wa Mapacha Watatu wakiwa pamoja na wachezaji na baadhi ya wanenguaji wa bendi tofauti.

No comments:

Post a Comment