Pages

Monday, February 6, 2012

SHEREHE ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 35 YA CCM MWANZA YAFANA


Rais Jakaya Kikwete akihutubia maelfu ya wana CCM na wakaazi wa Mwanza leo katika kuadhimisha miaka 35 ya CCM uwanja wa Kirumba (PICHA NA IKULU)
Wageni waalikwa mbalimbali kutoka nje ya nchi wamehudhuria katika maadhimisho hayo ya miaka 35 ta CCM mkoani Mwanza. (PICHA NA IKULU)
Mama Salma Kikwete na Spika Anne Makinda na wakinamama wakisherehekea miaka 35 ya CCM baada ya kukunwa na wimbo wa Vicky kamata. (PICHA NA IKULU)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akipokea salamu za heshima kutoka kwa gwaride la vijana wa CCM wakati wa sherehe hizo. Wengine kushoto ni Makamau Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Clement Mabina na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama. (Picha na Bashir Nkoromo).
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisalimia wananchi alipowasili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba katika kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM, leo. (Picha na Bashir Nkoromo)
Maelfu ya watu waliohudhuria sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza leo wakishangilia kwa furaha (Picha na Bashir Nkoromo)
Gwaride la Vijana wa CCM likipita kwa ukakamavu mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wakati wa sherehe za kilele hicho. Vijana 400 wameshiriki gwaride hilo (Picha na Bashir Nkoromo) Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akicheza muziki wa Suma Lee jukwaani. (Picha na Bashir Nkoromo)
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Suma Lee akionyesha umahiri wake alipopanda jukwaani kutumbuiza wakati wa sherehe hizo. (Picha na Bashir Nkoromo)

No comments:

Post a Comment