Pages

Tuesday, February 7, 2012

Urusi kujadiliana na Syria


Balozi wa Urusi kwa Umoja wa Mataifa akipiga kura ya turufu
Msimamo wa Urusi kuhusu matukio nchini Syria umeghadhabisha sana baadhi ya serikali za kimagharibi.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Hilary Clinton pamoja na chancellor wa ujerumani Angela Markel wameshutumu hatua ya Urusi na China ya kupiga kura ya turufu kupinga azimio la kuikosoa Syria katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Hatua hii ya Urusi itakuwa njia moja ya kuonyesha kwamba kuna njia nyingine ya kukabiliana na kusitisha mapigano yanayozidi kuongezeka nchini Syria.
Waziri wa masuala ya nje wa Urusi Sergei Lavrov hata hivyo hajabainisha wazi nini maazimio yake atakapokutana na rais Assad mjini Damascus akisema tu kwamba ametumwa na rais wake.
Hata hivyo ameelezea wazi msimamo wa Urusi akisema ni raia wa Syria wala sio jumuiya ya kimataifa ndio wana uwezo wa kuamua ni nani atakayekuwa rais wao.

No comments:

Post a Comment