Pages

Wednesday, February 8, 2012

WANAHARAKATI WAANDAMANA KUSHINIKIZA SERIKALI ICHUKUE HATUA JUU YA MGOMO WA MADAKTARI WA MUHIMBILI




      

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba akizungumza na waandishi wa habari katika maeneo ya Salender Brige, kuelezea maadamano ya wanaharakati hao ya kuishinikiza serikali kuchukua hatua na kutatua mgogoro wa mgomo wa Madaktari wa Hospitali ya Muhimbili, ulioanza hivi karibuni na ambao bado unaendelea. Ameongeza kwamba hali ya wagonjwa inaendelea kuwa mbaya zaidi kwa sababu ya mgomo huo, Dk Hellen Kijo-Bisimba mara baada ya kumalizika kwa maandamano hayo yaliyofanyika leo.
Mkurugenzi wa TAMWA, Analilea Nkya akiwa ameshikilia bango lake wakati wa maandamano hayo jijini Dar es salaam leo.
Polisi wakiwaamuru waandamanaji watawanyike mara baada ya kufika katika eneo la Salender Brige jijini Dar es salaam leo
         

No comments:

Post a Comment