Pages

Friday, March 23, 2012

KWA UZEMBE HUU WA UWANJA WA NDEGE NDULI SERIKALI ITAUNDA TUME?


Rais Jakaya Kikwete akitua katika uwanja wa Ndege Nduli mkoani Iringa juzi
Wananchi wakiwa wamejipanga kando kando ya uwanja wa ndege Nduli huku nyasi zikiwa zimewazidi urefu kumsubiri Rais Kikwete
Ndege ya Rais Kikwete akijiandaa kuruka katika uwanja wa Ndege Nduli huku ikiwa imefunikwa na nyasi ndege
Huu ni uwanja wa Nyasi za mifugo ama uwanja wa Ndege unaohitaji usalama wa hali ya juu?
Ndege ya Rais Kikwete akiingia katika eneo lenye nyasi
Huu ndio uwanja wa Ndege Nduli ambao usalama wake kwa viongozi ni mdogo zaidi
Nilishawahi kuandika katika mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com juu ya gari chakavu la uwanja wa ndege Nduli na leo naandika tena juu ya nyasi zinazohatarisha usalama wa viongozi wangu wa kitaifa ambao wanatumia uwanja huo na nitaendelea kuandika tena na tena .

Kwanza napenda kueleza masikitiko yangu kwa uongozi wa uwanja huo na wote wanaohusika na usimamizi wa viwanja vya ndege nchini kwa kushindwa kufyeka nyasi hizo ndefu na kuonyesha kuutelekeza uwanja huo .

Pamoja na kuelekeza masikitiko yangu kwa kundi hilo bado lawama nyingi kwa viongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa chini ya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa ambaye ni mkuu wa mkoa wa Iringa Dr.Christina Ishengoma na watu wa usalama wa Taifa kwa kutoliona hili.

Kwani binafsi nyasi hizo ndefu katika uwanja wa Ndege Nduli naona ni janga kubwa kwa taifa ambalo kwa sasa ni vigumu kuona madhara yake ila likitokea la kutokea ndipo janga hilo kuja kuonekana na hata kuundiwa tume kuchunguza tukio husika.

Ninasema hivyo kutokana na usalama wa viongozi wetu wanaotumia uwanja huu wa Ndege Nduli kuwa mdogo zaidi kwani waharifu wanaweza kutumia nyasi hizo kujificha na kutenda uharifu dhidi ya viongozi wetu .

Kiukweli naomba wahusika wote tuweze kulifanyia kazi suala hili ambalo ni hatari kwa usalama wa viongozi wetu kwani tumekuwa mabingwa wa kuunda tume za kuchunguza ajali zinapotokea ila katika hili la nyasi ndefu katika uwanja nalo tunasubiri kuundwa kwa tume kuja kuchunguza ?

No comments:

Post a Comment