Mwamuzi
Israel Mujuni pamoja na wasaidizi wake akitoka nje kwa kusindikizwa na
askali wa kikosi cha kutuliza Ghasia FFU mara baada ya kupuliza kipenga
cha mwisho kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliokutanisha timu ya
Yanga ya Jangwani na timu ya Azam FC kutoka Chamazi ambapo Yanga
imekandamizwa magoli 3-1 na wauza Sembe hao wa Chamazi kwenye uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
Mwanzo ulikuwa ni
mchezo mzuri uliokuwa wa vuta nikuvute kwa kila upande lakini mambo
yalibadilika mara baada ya Azam kuandika goli la kwanza, mchezaji Haruna
Niyonzima wa Yanga alionekana kumlalamikia refa mara kwa mara jambo
ambalo refa alimuonya mara kadhaa lakini, hata hivyo Niyonzima
aliendelea baada ya muda, alitolewa nje kwa kadi nyekundu, jambo
ambalo lilizua tafrani uwanjani huku makonde yakirushwa hovyo, baadae
naye mchezaji Nadir Haroub Canavaro alipewa kadi nyekundu kutokana na
vurugu hizo na kuzua tifu lingine uwanjani.
Hali ilikuwa kama hivi angalia matukioo ya picha hizi.
No comments:
Post a Comment