Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe
meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utunzi
bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora
Kilimanjaro Music Award 2012 zinazofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na
wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania na nje ya nchi.
Msanii Nassib Abdul ‘Diamond’
usiku wa jana ameng’ara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award, baada ya
kujinyakulia tuzo tatu.
“Namshukuru Mungu, wakati
mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru
Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo ninachukua tuzo ya tatu sasa
hivi, alisema Diamond baada ya kushinda tuzo ya Video Bora ya
Mwaka, kupitia wimbo Moyo Wangu, ambayo ilikuwa ya tatu usiku huu.
Diamond alizishinda nyimbo za Hakunaga
ya Suma Lee, Wangu ya Jay Dee, Ndoa Ndoana ya Kassim na Bongo Fleva ya Dully Sykes.
Mwanamuziki Diamond akipiga picha na mama yake wa pili kutoka kushoto
na Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka kutoka kulia pamona na wanenguaji wake
mara baada ya kupokea tuzo yake ya utuzni bora wa nyimbo.
Mwimbaji wa muziki wa Taarab ambaye ameshinda tuzo ya mburudishaji bora
kwa wanawake Malkia Khadija Omar Kopa akitumbuiza katika hafla hiyo
usiku huu.
Malkia Khadija Omar Kopa akishukuru wapenzi wake mara baada ya kushinda
tuzo ya mburudishaji bora, wa pili kutoka kushoto ni mume wake na
wengine ni watoto wake.
Watoto wa Malkia wa Mipasho Khadija Omar Kopa wakishuka jukwaani mara
baada ya kumtunza mama yao wakati alipokuwa akitumbuiza katika hafla
hiyo.
Kulia ni Msanii Profesa Jay na kushoto ni Mkubwa Fella meneja wa kundi
la TMK Family wakimkabidhi tuzo Roma Msanii wa muziki wa Hiphop
aliyejishindia tuzo ya msanii bora wa Hiphop.
Burudani kutoka THT
Burudani kwa nguzu zote.
No comments:
Post a Comment