KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa |
Ibrahim Yamola
KATIBU
Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amewajibu jeshi la polisi mkoani
Mwanza kuwa, anawakaribisha wote wanaotangaza kutaka kumkamata kufuatia
madai ya kutoa kauli za uchochezi katika mkutano wake wa hadhara
uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, kutangaza kumchukulia hatua za kisheria Katibu Mkuu huyo .
Akiwa
katika mkutano huo uliofanyika kwenye Viwanja vya Sahara, Dk Slaa
alitoa wiki moja kwa Jeshi la Polisi mkoani humo kuwakamata wale wote
waliohusika na vurugu katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kirumba
uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu.
Ilidaiwa
kuwa vurugu hizo ambazo zilihusisha wafuasi wa CCM, zilisababisha
kujeruhiwa vibaya kwa wabunge wa Chadema, Samson Kiwia wa Ilemela na
Salvatory Mchemli wa Ukerewe.
Katika
mkutano huo, Dk Slaa alisema kama Jeshi la Polisi halitawakamata
watuhumiwa na kuwachukulia hatua za kisheria ndani ya siku saba, yeye
mwenyewe atachukua jukumu la kuwahamasisha wananchi wa Mwanza kuwakamata
vijana hao.
Lakini
jana baada ya kuulizwa kuhusu kuchukuliwa hatua na Polisi Dk Slaa
alisema, “Nalikaribisha Jeshi la polisi wakati wowote kuja kunikamata
na nitafurahi kwa kuwa nafanya hivi kwa ajili ya kutetea haki za
watanzania wanaoporwa uhuru wao na jeshi lao,”.
Mgombea
huyo wa Urais kwa tiketi ya Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 ,
aliwataka polisi kabla ya kumkamata yeye waanze kuwakamata waliohusika,
kuwakamata askari waliokuwapo katika eneo la tukio wakati wabunge wa
Chadema wakishushiwa kipigo.
“Haiingii
akilini uhalifu unafanyika na polisi wako katika eneo hilo halafu
wasiwakamate watuhumiwa, kuna nini hapa katikati? Alihoji Dk Slaa.
Habari kwa hisani ya Vijimambo blog
Alisema
jeshi hilo linatakiwa kutambua tofauti ya uchochezi na kukemea kwani
anachokifanya ni kueleza ukweli kwa kuwa alikuwa na majina yote ya
watuhumiwa pamoja na magari yaliyotumika katika tukio hilo.
“Kama watashindwa kulifanyia kazi kwa wakati tutawasemea kwa wananchi ili wachukue hatua wenyewe” alisisitiza Dk Slaa.
Dk
Slaa alifafanua udhaifu wa Polisi kwamba wamekuwa wazito kufuatilia
taarifa za hatari zinazotolewa na wananchi hasa kunapotokea matukio
yanayohatarisha utulivu na amani.
“Tulishatoa taarifa kwa polisi kuwa mkoani Mbeya kuna mtu anatengeneza Dola za Marekani lakini jeshi hilo,” alitoa mfano Dk Slaa
Aliongeza,
“Harakati hizi hazitakwisha hadi pale Tanzania itakapopata uhuru kwa
wananchi kutosingiziwa kesi, hata tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 50 ya
watuhumiwa wanabambikiwa kesi na polisi”.
Hatua
hiyo ya jeshi la polisi kutangaza kumchukulia hatua Dk Slaa imekuja
baada ya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Philipo Kalangi kusema
kauli zilizotolewa na Katibu mkuu huyo wa Chadema ni za uchochezi
ambazo zinaweza kuharibu amani ya nchi.
Kamanda Kalangi alisema Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na si kwa matakwa ya mtu binafsi.
Habari kwa hisani ya Vijimambo Blog
Habari kwa hisani ya Vijimambo Blog
No comments:
Post a Comment