Mwanamuziki
wa Hip hop mwenye mafanikio ya aina yake katika industry ya muziki wa
kibongo, Hamis Mwinjuma a.k.a MwanaFA ameondolewa kwenye list ya watu
ambao walipaswa kuchanwa kwenye volume three ya Anti-Virus ya Vinega.
MwanaFA
ambaye alikuwa centre ya michano katika volume iliyopita iliyopata
mafanikio makubwa, safari hii ameondolewa kwenye hiyo list baada ya
kujitoa rasmi TFU ambayo ni kampuni ya wasanii yenye dhamana ya
kusimamia inayosemekana studio iliyotolewa na mwenye nchi yake. TFUama
Tanzania Fleva Unit na ilipata wakati mgumu sana pale Mh Sugu
alipoilipuwa bungeni huku umati wa Tanzania ukikodoa macho kwenye kideo.
Akizungumza
na KaribuNdani Kinega kiongozi Peenlawyer amesema Mwana FA sio target
tena kwani kashajitoa TFU ila moto utawaka kwa Kusaga, Nchimbi na
utawaka zaidi kwa Ruge, mameneja masoko, Kili Awards na baadhi ya
watangazaji ambao wamekuwa chachu ya rushwa na unyanyasaji wa wasanii..
Volume 3 iko njiani na kinachofanywa kwa sasa ni kujipanga ili kuangalia muda muafaka wa kudondosha hiyo mix-tape.
No comments:
Post a Comment