Mbunge
wa jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama cha CHADEMA Mh. Tundu Lissu
(mwenye fimbo) akiingia kwenye viwanja vya kituo cha zamani cha mabasi
mjini Singida kwa kuhutubia wananchi.
Mbunge
wa jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA) muda mfupi kabla hajaanza
kuhutubia wakazi wa jimbo la Singida mjini. Wa kwanza kulia ni mke wake.
Mbunge
wa viti maalum kupitia Chama cha CHADEMA na ambaye ni mdogo wake Tundu
Lissu Christina Mughwai, akisalimia mamia ya wananchi waliohudhuria
mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya Tundu.
Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA) Mh. Tundu Lissu akihutubia wakazi wa jimbo la Singida mjini.
Mbunge
wa jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA) Mh. Tundu Lissu (waliosimama
mwenye kofia) akitoa salamu ya CHADEMA ya ‘peoples power’. (Picha zote
na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mbunge
wa jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA) Mh. Tundu Lissu, amedai kwamba
zaidi ya shilingi milioni 200, zimetumika kugharamia kesi ya ‘kuunga
unga’ ambayo ililenga kutafuta kichwa chake kama ilivyokuwa kwa Yohana
Mbatizaji.
Bila
kufafanua kuwa kichwa chake kilikuwa kikitafutwa kikiwa kimetenganishwa
na kiwiliwili au kikiwa hakijatenganishwa na kiwili wili chake, amesema
kati ya kesi 14 zilizofunguliwa katika mahakama tofauti nchini, kwa
ajili ya kutengua matokeo ya wabunge wa CHADEMA ya kwake ilikuwa kubwa
zaidi na ndio maana haikupewa umuhimu unaostahili na vyombo vya habari.
Hata
hivyo, hakufafanua au kueleza iwapo hivyo vyombo vya habari navyo
vilinufaika na kiasi hicho cha shilingi milioni 200 ambazo zililenga
kumwangamiza kisiasa.
Tundu
amesema wana-CCM hao ambao ni wakulima wa kawaida, wametumiwa na
wahusika walikuwa wakimwaga fedha ili kufanikisha azma zao ya kumng’oa
katika nafasi yake ya ubunge, lakini fedha zote zimeliwa bila
kufanikisha lengo.
Aidha,
alisema kuwa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM Yusufu Makamba, aliwahi kutoa
waraka kuwa katika majimbo yote yaliyochukuliwa na vyama vya
upinzani,wahusika walioshindwa,wafungue kesi mahakamani.
Habari kwa Hisani ya Mo Blog
Habari kwa Hisani ya Mo Blog
No comments:
Post a Comment