Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, April 26, 2012

TIMU YA AL-AHLY SHANDY YA SUDAN YATUA BONGO KUWAKABILI SIMBA



Baadhi ya wachezaji wa timu ya Al-Ahly ya Sudan, wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,leo kwa ajili ya kukipiga na Simba, siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Picha na Stori kwa hisani ya fredy njenje blog.
****************************
TIMU ya Al-Ahly ya nchini Sudan, imewasili nchini leo ikiwa na msafara wa watu 30 wakiwamo wachezaji na viongozi wa timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Simba, ambapo mgeni rasmi katika mchezo huo ametajwa kuwa anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
 
Timu hizo zitakwaana Aprili 29 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa 16 bora ya kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF).
Akizungumza baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa JK Nyerere, Kocha mkuu wa timu hiyo, Kouk Mohammed, alisema kuwa mchezo huo uantarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kuwaona Simba katika baadhi ya michezo yao huku akilinganisha na timu yake.
Aidha alisema anaifahamu Simba kama moja ya timu mahiri Barani Afrika sambamba na kuwa na uzoefu wa kucheza michuano ya kimataifa hali ambayo itawafanya wawe makini zaidi watakaposhuka dimbani.
Hata hivyo kocha huyo raia wa Tunisia alisema kwamba huenda wakaathiriwa na hali ya hewa ya Tanzania kutokana na kuwa tofauti na Sudan ingawa alisema watajitahidi kukabiliana nayo.
Kikosi cha Al Ahly kinaundwa na wachezaji watano wa kimataifa wakiwemo wawili kutoka Nigeria , mmoja kutoka Mali huku wachezaji wawili wakiichezea timu ya Taifa ya Sudan .
Al Ahly wanakutana na Simba baada ya kuitoa Ferroviario ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 3-0, huku Simba iliitoa Es Setif ya Algeria huku Simba ikibebwa na bao la ugenini baada ya nyumbani kushinda 2-0 kabla ya kwenda kufungwa 3-1.
Katika hatua nyingine tiketi kwa ajili ya kushuhudia mpambano huo zinatarajiwa kuanza kuuzwa leo katika vituo tofauti jijini Dar es salaam huku waamuzi wa mchezo huo kutoka Swaziland, Nhleko Simanga Pritchard, Mbingo Petros Mzikayifani,Sibandze Thulani, Fakudze Mbongiseni Elliot na Kamishna wa Kayijuga Gaspard wa Rwanda wanatarajiwa kuwasili leo.
 
Katika kujiandaa na mchezo huo, Simba imepiga kambi eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam ambapo kocha mkuu wa Simba Mserbia Milovan Cirkovic amejigamba kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili zijazo katika jiji la Shandy , Sudan .

No comments:

Post a Comment