Baadhi
ya wachezaji wa timu ya Al-Ahly ya Sudan, wakiwasili kwenye Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,leo kwa ajili ya kukipiga na Simba,
siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Picha na
Stori kwa hisani ya fredy njenje blog.
****************************
TIMU
ya Al-Ahly ya nchini Sudan, imewasili nchini leo ikiwa na msafara wa
watu 30 wakiwamo wachezaji na viongozi wa timu hiyo kwa ajili ya
kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Simba, ambapo mgeni rasmi katika
mchezo huo ametajwa kuwa anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu,
Frederick Sumaye.
Timu
hizo zitakwaana Aprili 29 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
katika mchezo wa kwanza wa 16 bora ya kombe la Shirikisho Barani Afrika
(CAF).
Akizungumza baada
ya kuwasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa JK Nyerere, Kocha mkuu wa
timu hiyo, Kouk Mohammed, alisema kuwa mchezo huo uantarajiwa kuwa na
ushindani mkubwa kutokana na kuwaona Simba katika baadhi ya michezo yao
huku akilinganisha na timu yake.
Aidha
alisema anaifahamu Simba kama moja ya timu mahiri Barani Afrika
sambamba na kuwa na uzoefu wa kucheza michuano ya kimataifa hali ambayo
itawafanya wawe makini zaidi watakaposhuka dimbani.
Hata
hivyo kocha huyo raia wa Tunisia alisema kwamba huenda wakaathiriwa na
hali ya hewa ya Tanzania kutokana na kuwa tofauti na Sudan ingawa
alisema watajitahidi kukabiliana nayo.
Kikosi
cha Al Ahly kinaundwa na wachezaji watano wa kimataifa wakiwemo wawili
kutoka Nigeria , mmoja kutoka Mali huku wachezaji wawili wakiichezea
timu ya Taifa ya Sudan .
Al
Ahly wanakutana na Simba baada ya kuitoa Ferroviario ya Msumbiji kwa
jumla ya mabao 3-0, huku Simba iliitoa Es Setif ya Algeria huku Simba
ikibebwa na bao la ugenini baada ya nyumbani kushinda 2-0 kabla ya
kwenda kufungwa 3-1.
Katika
hatua nyingine tiketi kwa ajili ya kushuhudia mpambano huo
zinatarajiwa kuanza kuuzwa leo katika vituo tofauti jijini Dar es
salaam huku waamuzi wa mchezo huo kutoka Swaziland, Nhleko Simanga
Pritchard, Mbingo Petros Mzikayifani,Sibandze Thulani, Fakudze
Mbongiseni Elliot na Kamishna wa Kayijuga Gaspard wa Rwanda
wanatarajiwa kuwasili leo.
Katika
kujiandaa na mchezo huo, Simba imepiga kambi eneo la Kidongo Chekundu
jijini Dar es Salaam ambapo kocha mkuu wa Simba Mserbia Milovan
Cirkovic amejigamba kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira
mazuri kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili zijazo katika
jiji la Shandy , Sudan .
No comments:
Post a Comment