Singida
WATU wane wamelazwa hospitali ya Mkoa Singida, baada ya basi la Mohamed Trans, kugongana na basi dogo, mjini Singida.
Kamanda wa Polisi mkoa
Singida, Celina Kaluba, amesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva
basi la Mohamed Trans, aliyejaribu kuingia katika barabara kuu ya
Mwanza- Dodoma, bila kuchukua tahadhari yoyote.Hata hivyo dereva wa basi
la Mohamed Trans ambaye jina lake halikupatikana, alitoroka.
Majeruhi waliolazwa ni
Yesaya Samson(dereva wa basi dogo) aliyevunjika miguu yote, Paulo
Rajabu, Parick Stephano na William Richard, waliopata majeraha sehemu
mbalimbali za miili yao.
Abiria zaidi ya 50
waliokuwa kwenye basi la Mohamed Trans hawakupata madhara, huku wenzao
wanne wa waliojeruhiwa na kulazwa walikuwa abiria wa basi dogo.
Ajali hiyo imehusisha
basi namba T 848 BEQ Scania, kampuni ya Mohamed Trans likitoka Morogoro
kwenda Mwanza na basi lingine dogo namba T 499 BRS Dyana, likitokea
Singida mjini, kwenda kijiji cha Iglansoni, Singida vijijini.
Kutokana na ajali hiyo,
Kaluba amewakumbusha madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani,
ili kuepusha ajali zisizokuwa za lazima.
No comments:
Post a Comment